loader
Picha

Wafugaji toeni chanjo kwa wanyama

Kuna wanaofuga mifugo mbalimbali ambapo baadhi yao hupendelea mifugo aina ya mbwa, paka, mbuzi, ngombe, kondoo na hata nguruwe.

Mifugo yote inahitaji kuangaliwa afya zao na kwani inaweza kuwa na magonjwa ambayo ni hatari kwa ustawi wa maisha ya binadamu.

Mbali ya mifugo hiyo kupata magonjwa na kusababisha vifo na hasara kwa mfugaji, hutokea pia ukosefu wa chanjo kukwamisha maendeleo yatokanayo na sekta hiyo ya mifugo.

Kwa mfano ufugaji wa mbwa ni moja ya ufugaji unaopendwa na wananchi wengi wakiamini mbwa ni moja ya mfugo unaoweza kutoa ulinzi katika makazi ya watu kwa njia mbalimbali.

Wakati jamii ikiamini mbwa anaweza kuwa mlinzi mzuri katika makazi yao, bahati mbaya amekuwa mnyama ambaye kwa namna moja au nyingine, afya yake husahaulika kufuatiliwa.

Hatua zote zinazotakiwa mbwa kupewa chanjo mara kadhaa husahaulika wakati akiwa anapendwa na watoto wengine bila kufahamu athari wanazoweza kuzipata kama ana ugonjwa.

Ikumbukwe mbwa anaweza kuambukiza ugonjwa mbaya wa kichaa cha mbwa ambao aliyeng’atwa na mnyama huyo anahitaji kupatiwa chanjo haraka iwezekanavyo ili kumuepusha na kifo kutokana na ugonjwa huo.

Katika kudhibiti ugonjwa huo kwa wilaya ya Moshi, Shirika la Kimataifa la Chakula Duniani (FAO) likishirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID) hivi karibuni limetoa msaada wa chanjo za mbwa dozi 33,700 zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 103.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi Mkazi wa FAO, Fred Kafeero alisema ugonjwa huo huambukiza kwa njia ya mnyama mwenye kichaa cha mbwa kwa kumng’ata binadamu au wanyama wengine pia kuwepo kwa uwezekano wa kuambikizwa kichaa baada ya kuumwa na mbwa asiyeonesha dalili za ugonjwa huo.

Anasema kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa zaidi ya watu 70,000 hufariki kila mwaka kwa ugonjwa huo na Tanzania tafiti mbalimbali zinaonesha watu 1500 hufariki kila mwaka kwa ugonjwa huo.

Mfano kwa mnyama mmoja, ni muhimu kwa wafugaji wa wanyama kuhakikisha wanatoa chanjo kwa mifugo yao yote kwani wapo wanaoacha mifugo ikizurura katika mitaa mbalimbali huku kukiwa na fursa ya kubeba magonjwa yenye hasara kwao na taifa pia.

Ni muhimu wafugaji kufahamu gharama za kutotoa chanjo kwa mifugo hiyo na kumtibu mgonjwa mmoja wa kichaa cha mbwa ni Sh 90,000 huku kuchanja mbwa mmoja ikigharimu Sh 14,000, hivyo chanjo ni bora na nafuu zaidi.

Shime wafugaji wasibague aina ya wanyama watakaowapa chanjo. Waone ni jambo la lazima kufanya hivyo kuwezesha kuwepo maendeleo kwa taifa na mtu mmoja mmoja kwa ujumla.

NYOTA ya kijana wa Mbagala, Mbwana Samatta ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi