loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wahalifu mtandaoni wanavyotumia ujumbe wa mapenzi kunasa watu

Lakini hali iko hivi: Saa 12:30 asubuhi zaidi ya wavulana 20 wenye umri kati ya miaka 14 na 18, wengi wao wakiwa wamekatisha masomo, wanazunguka nje ya ofisi zinazotoa huduma ya mtandao kwa kulipia.

Muda mfupi baadae, mmiliki wa ofisi moja anafungua mlango. Vijana wote waliokuwa nje ya mlango huo wanaingia ndani kwa kugombania na kisha kuvamia kompyuta zilizopo.

"Wanakaa hapa kutwa nzima wakati mwingine mpaka saa nne usiku wakati wa kufunga. Wengine wanakosa muda wa kula au kunywa kwa kuhofia mtu mwingine atachukua nafasi. Wanachokifanya ni kuwapigia simu rafiki zao wa kike ili walete chakula na vinywaji,” anasema Jean Luc Tiemele mmiliki ofisi inayotoa huduma ya mtandao inayopendwa na vijana wengi wa Ivory Coast.

"Binafsi sifahamu jinsi wanavyofanya, lakini naona wanavyovuna maelfu ya anuani za barua pepe kwa siku. Wanatuma barua pepe zisizo na idadi kwa ajili ya madodoso ya kibiashara kupitia anuani hizo.

"Mara baada ya kupata majibu, wanaendelea kumfuatilia mtu aliyejibu hadi atoe pesa. Kiasi cha pesa wanachopata hutumia kuwarubuni wasichana, kununua simu za mkononi za gharama, saa, manukato, vinywaji na wakati mwingine magari,” anasema Tiemele.

Hadithi hii inafanana na hadithi nyingine zinazotokea karibu katika kila sehemu inayotoa huduma ya mtandao kama kwa Tiemele, katika miji kadhaa ya nchi ya Ivory Coast yenye watu milioni 6. Wanaofanya vitendo hivi wanafahamika kama wahalifu wa mtandaoni ambao hutumia siku saba za wiki mbele ya kompyuta kujitafutia fedha za haraka haraka.

"Huwezi kukuta sehemu ya kutolea huduma ya mtandao jijini Abijan, nchini Nigeria bila wahalifu hawa,” anasema Armand Zadi, mwanzilishi wa asasi inayofanya kampeni ya kutokomeza uhalifu huo katika nchi za Afrika Magharibi.

"Wamekatisha masomo na wanaamini watafanikiwa maishani kupitia mtandao. Kwa sababu wanaona vijana wadogo mjini wanatumia fedha zilizotokana na vitendo hivyo. Wasiwasi wetu wataleta picha mbaya kwa vijana wengine wanaokua,” anasema Zadi. Serikali ya Ivory Coast imeanzisha kitengo kipya katika Jeshi la polisi.

Kinachoundwa na polisi, wataalamu wa kompyuta na mawasiliano, wanasheria kwa ajili ya kufanikisha mkakati wa kuwakamata wahalifu ambao wameharibu jina la nchi hiyo kwa nchi nyingine duniani.

Ripoti ya mwaka ya kitengo hicho inaonesha waathirika wa vitendo hivyo wamepoteza milioni 6.2 mwaka 2012 na milioni 6.6 kwa mwaka 2013 nchini humo. Jumla ya milioni 28 zimepotea tangu kitengo hiko kilivyoanza kuweka kumbukumbu ya taarifa za uhalifu miaka mitano iliyopita. Ni jambo baya pia kwa uchumi wa nchi, sekta ya uwekezaji na utalii.

Kama hakuna kitu kitakachofanyika kukomesha uhalifu huo, tatizo litaendelea kukua na kufukuza wawekezaji na hata kuharibu sifa ya nchi ya kuwa kinara wa uzalishaji wa kokoa duniani, anasema Ouattara Mkuu wa kitengo hicho.

“Tukumbuke kuwa, watu wengi wanaoathirika na vitendo hivi wanatoka Afrika Magharibi, lakini ripoti inaonesha raia wa Ivory Coast ndio wanaoathirika kila kukicha. Kwa hiyo ni tatizo kubwa a tunawajibika kulitatua,” anasema Quattara.

Kitengo hicho kimepokea malalamiko 514 kutoka kwa waathirika wa mwaka 2013 kati yao asilima 42 ni kutoka sehemu za vijijini. Na kitengo kimefanikiwa kukawamata washtakiwa 50 ambao wamefunguliwa mashtaka.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, zaidi ya nusu ya waathirika hao wamenaswa baada ya kutumiwa ujumbe unaohusu mapenzi. Wakati ujumbe wa kazi umeathiri kwa asilimia 10 na asilimia saba ni ujumbe ambao haukutambuliwa.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa wahalifu hutuma ujumbe wa mapenzi unaomshawishi mlengwa aendelee kufanya mawasiliano na baadae hurubuniwa kiasi cha kumpa pesa kwa mhalifu.

“Nilikuwa natuma fedha mara kwa mara mpaka nilipogundua kuwa natapeliwa ndio niligundua kuwa sio msichana ila ni mwanaume," anasema Steve Widmer muathirika wa wizi wa mtandaoni aliyeko Uswisi.

“Mara ya kwanza ilikuwa rahisi sana, nilikuta barua pepe kwenye akaunti yangu. Alikuwa ananifahamisha kuhusu fursa za uwekezaji nchini Ivory Coast na jinsi atakavyonisaidia kupata leseni ya bei nafuu na kwa muda mfupi kwa ajili ya kuendeshea biashara nchini humo,” anasema Widmer.

“Wakati mwingine alikuwa akinitumia kiasi cha fedha kwa njia ya kifurushi, ili nitume nyaraka zangu muhimu haraka, ili amkabidhi mjomba wake anayefanya kazi Wizara ya Biashara, jambo ambalo nilifanya. Kwa ujumla tuliendelea na mipango kwa mwaka mmoja bila kukutana.

"Niliendelea kumtumia fedha kwa ajili ya mambo mbalimbali mpaka nilipogundua kuwa ananitapeli,” anasema.

Polisi wa Uswisi na Ufaransa kwa kushirikiana na kitengo hicho kimefanikiwa kufichua taarifa za simu, na hivyo kusaidia kuwakamata idadi kubwa ya vijana wa kike na wa kiume nchini humo.

Mmoja kati ya waathirika anayeishi nchini Switzerland anasema amepoteza kisasi kikubwa cha fedha alichoweka kwa ajili ya akiba kwa sababu ya wahalifu wa nchini Ivory Coast. Ouattara anasema watuhumiwa wengine bado wanafanyiwa upelelezi “Huwezi kumkamata kila mtu anayekaa mbele ya kompyuta. Timu yangu ya kazi inaheshimu haki za binadamu. Tunahakikisha hatumkamati mtu mpaka upelelezi ukamilike.”

Matumizi ya vitambulisho vya bandia, namba za simu za uongo na majina ya uongo ni miongoni mwa sababu zinazokwamisha upelelezi, anasema Ouattara.

“Tunatakiwa kutumia njia mpya na za kisasa zikiwemo simu zinazoonesha data kuhusu mhalifu, jambo ambalo linachukua siku na miezi mingi.”

Mwaka 2012, kampuni zote za mkononi za mkononi na zinazotoa huduma ya mtandao nchini Ivory Coast walitakiwa kusajili wateja wao ili iwe rahisi kuwafuatilia wakati wowote.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano inayosimamia sekta hiyo, zaidi ya watu milioni 17 walisajiliwa sawa na asilimia 92.8 ya watu milioni 22 wanaotumia mtandao.

Awali nchi hiyo haikuwa na sheria ya kuwachukulia hatua wahalifu wa mtandaoni, lakini mwaka 2013 serikali ili saini miswada miwili kuhusu uhalifu kwa njia ya mtandao na kudhibiti taarifa binafsi.

Adhabu ya makosa hayo ni kifungo cha kati ya mwaka mmoja hadi 20 jela au kulipa faini ya kati ya dola 1,000 hadi dola 200,000.

Sylvie Kouassi ( 37) mfanyabiashara anasema amepoteza dola 4,200 kwa mhalifu aliyeko jijini Abijan baada ya kufungua akaunti yake kwenye ofisi inayotoa huduma ya mtandao kwa kulipia. Anasema siku hiyo aliingia kwa ajili ya kuweka sawa mipango yake ya fedha zinazotoka nje ya nchi.

"Nilipofika kwa wakala wa kutoa fedha niliambiwa hela zangu zimeshatolewa.Nikagundua kuwa kompyuta niliyotumia siku hiyo iliwekewa mtego na wahalifu wa mtandaoni,” anasema Kouassi.

Wanachokifanya wahalifu hao ni wanaweka programu maalumu za kunukuu au kurudisha namba za siri na anuani za barua pepe kwenye kompyuta mbalimbali hasa zinazotumiwa na watu wengi kwa ajili ya kuangalia taarifa muhimu kama za fedha, anasema Silvestre Moke, mhandisi wa masuala ya mtandao jijini Abidjan.

"Jambo la haraka na la msingi ni kuepuka mara moja kwenda kwenye sehemu zinazotumiwa na watu wengi kwa ajili ya kuangalia taarifa zako. Wana uwezo wa kufuatilia taarifa zako kwa siku au miezi bila wewe kujua,” anasema Moke. Kwa upande wake mmoja kati ya wahalifu ambaye hakutaja jina lake anasema, uhalifu wa mtandaoni barani Afrika si uhalifu asilia bali ni mabaki ya ukoloni.

"Ni kweli kwamba baadhi ya ndugu zetu wananasa kwenye mtego, lakini nia hasa ni watu kutoka nchi za Magharibi.Hatuna kazi, taasisi za fedha hazitupi mkopo kwa ajili ya biashara, unadhani nini cha kufanya ili tuweze kuishi? Zamani kaka zetu walikuwa wakisafiri kwenda Ulaya kutafuta maisha lakini sasa hivi ubalozi hautoi vibali tena. Mtandao ni fursa nyingine kwa vijana wa Kiafrika kijikomboa kiuchumi,” anasema mhalifu huyo.

Makala haya yameandikwa na Kiyao Hoza kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya habari.

WATANZANIA kama walivyo watu wa mataifa ...

foto
Mwandishi: Kiyao Hoza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi