loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wahudumu hawa wasifumbiwe macho

Tunasema ni ya kuungwa mkono kwa vile, viongozi wa Serikali pamoja na NHIF, wana nia njema ya kuona Watanzania wanachama na mfumo uliopo wa kutoa fedha zao mfukoni kila waendapo hospitalini, kupata huduma na dhamira ni kufikia asilimia 30 ya Watanzania, kuwa na bima ya afya ifikapo mwaka 2015.

Juhudi hizi haziwezi kufikiwa, ikiwa baadhi ya wahudumu katika baadhi ya vituo vya afya vya binafsi na vya Serikali, wataachwa bila kukemewa kuwadhalilisha wenye kadi za NHIF, kwa kuwa wanakuwa wanawavunja moyo.

Sadiki aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika hotuba yake, iliyosomwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na NHIF kwa wadau wa mfuko huo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakiwemo wanasiasa, viongozi wa dini, taasisi, wabunge, wakuu wa wilaya na wengineo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa, matumizi ya kadi kwa ajili ya utoaji wa huduma mbalimbali, yanaendelea kushika kasi duniani kote, lakini kumekuwa na dhana potofu miongoni mwa baadhi ya watoa huduma, kuthamini wagonjwa wanaotoa fedha taslimu na kuwadharau wale wanaotumia kadi za bima ya afya.

Akasema lazima tabia hii ikome mara moja na ni lazima watambue kwamba mkakati wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kwamba kila Mtanzania, anakuwa na bima ya afya na kupunguza utaratibu wa wagonjwa kutoa fedha taslimu kwa namna moja au nyingine.

Nasi tunaungana na rai ya Mkuu wa Mkoa, aliyoitoa kwa wanachama wa mfuko, kutoa taarifa mara wanapobaini uwepo wa udhalilishaji huo.

Ni lazima wahudumu katika vituo vya huduma, watakaobainika kuwadhalilisha wagonjwa kwa kigezo cha kutumia kadi ya bima ya afya, waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Wakati juhudi za NHIF zimekuwa zikilenga kuhakikisha Watanzania wengi, wanafikiwa na huduma ya Bima ya Afya, ni kweli kumekuwepo na malalamiko ya hapa na pale kutoka kwa wanachama, wakidai kunyanyaswa na watoa huduma katika baadhi ya hospatali na vituo vingine vya afya. Zipo baadhi ya hospitali, zinafanya vizuri kwa kutenga eneo la wenye kadi wa NHIF.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu wa NHIF, Dk Lekey Frank, kuna baadhi ya hospitali waganga na wahudumu wa afya, wanapenda kuhudumia zaidi eneo lililotengwa kwa ajili ya wanachama wa bima ya afya.

Alisema hayo wakati akiwasilisha mada katika warsha, iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo.

Dk Frank alisema katika maeneo mengi katika baadhi ya hospitali zetu hapa nchini kwa sasa, madaktari na wahudumu wangependa kupangwa huko penye wanachama NHIF.

Tunaamini, hospitali nyingine nyingi, zitaiga mfano wa zile ambazo tayari wahudumu wa afya, wanaona umuhimu wa kuwahudumia wenye kadi na watenge maeneo kwa ajili ya wenye kadi ili kuondoa usumbufu huu.

UCHAGUZI Mkuu wa madiwani, wabunge, wawakilishi, Rais wa Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi