loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wajasiriamali Kibaha wamshukuru Kikwete

Kutokana na kutafutiwa masoko hayo ya nje ya Tanzania imesaidia kuinua kipato cha wajasiriamali hao ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakihangaika kupata masoko hayo.

Akizungumza mjini hapa, mmoja ya wajasiriamali hao ambaye ni Mkurugenzi wa Pallangyo General Supply, Maria Pallangyo alisema kuwa kutokana na Rais kuwatafutia masoko ya nje kwa sasa bidhaa zao zimekuwa zikinunuliwa kwa wingi baada ya kuzitangaza.

Pallangyo alisema kuwa wao kwa upande wake na wenzake wanasindika vyakula ambavyo ni chakula, tiba na lishe, ambavyo ni dawa kwa ajili ya magonjwa mbalimbali ambayo yanatokana na ulaji mbaya wa vyakula na usasa wa maisha.

“Kwa sasa tunashiriki maonesho mbalimbali ya bidhaa zetu kwenye nchi mbalimbali barani Afrika na baadhi wanakwenda hadi Ulaya hivyo ni jambo la kufurahisha kuona kiongozi wa nchi anawatafutia fursa za kuboresha maisha wananchi wake sehemu mbalimbali za dunia,” alisema Pallangyo.

Hata hivyo, alisema serikali ingeangalia uwezekano wa kuzishawishi taasisi za kifedha kupunguza riba ya mikopo wanayoitoa ili wajasiriamali waweze kukopa.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi