loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakazi wa vijiji vitatu waamriwa wasiondoke

Alitoa uamuzi huo wakati wa kikao chake na wajumbe wa halmashauri ya Wilaya ya Mafia baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa mwekezaji huyo amekuwa akiwanyanyasa wananchi wa vijiji hivyo.

Akiulizwa swali, Mohamedi Faki alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu mgogoro huo wa ardhi baada ya mtu aliyemwita mwekezaji kudai eneo la vijiji vitatu ni mali yake ambapo tayari wananchi wameshakaa hapo muda na mrefu na wamejenga.

Kinana alisema, haiwezekani mtu atelekeze shamba kwa muda mrefu halafu baada ya kuoana ardhi imekuwa na thamani, arejee na kudai eneo hilo ni lake.

“Si aliondoka mwenyewe, haiwezekani amiliki eneo hilo tangu mwaka 1949, na bila kuliendeleza. Nasema vijiji hivyo visiondolewe, kama kuna eneo litabaki basi hilo ndilo apewe,” alisema.

Vijiji vilivyomo katika shamba la minazi la Tumaini ni Baleni, Ndagoni na Kilogwe. Kinana aliwaahidi wananchi hao kuwa atalifuatilia suala hilo kwa Rais jakaya Kikwete ili kuhakikisha wananchi hao wanapata haki yao.

Mmiliki wa shamba ekari 4,000 (Tumaini) hana haki ya kumiliki eneo hilo baada ya kulitelekeza kwa zaidi ya miaka 20.

Awali, akitoa maelezo, Mkuu wa Wilaya ya mafia Sauda Mtondoo alisema Tumaini ana hati ya umiliki wa shamba hilo tangu mwaka 1949, na kueleza kuwa kwa muda mrefu alilitelekeza shamba hilo.

Alisema baada ya Uhuru, sehemu ya shamba hilo iligawiwa kwa kata tatu za Baleni, Ndagoni na Kilogwe ambapo kumejengwa shule, kanisa misikiti na makazi ya watu.

“Mwaka jana mtu huyo ameibuka na kusema yeye ni mmiliki halali wa eneo hilo na kuwa amekuja kufufua mipaka ambayo inapelekea vijiji vitatu kuwa ndani ya eneo lake.

Alisema kutokana na tatizo hilo serikali iliamua kumuamuru mtu huyo kuacha kufufua mipaka ya shamba hilo mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na kuwa tayari imeshapelekwa kwa rais kwa maamuzi zaidi.

Aidha, wananchi wa Mafia wameiomba serikali kusaidia kujenga vyuo vya ufundi(VETA) ili vijana wanaoshindwa kuendelea na elimu ya juu wapate mafunzo.

Rais Dk John Magufuli amewataka wawekezaji wenye nia ya ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi