loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakorofi Yanga kutimuliwa

Maamuzi hayo yametolewa jana baada kamati hiyo inayoundwa na wenyeviti wa matawi ya klabu hiyo kukutana Jumamosi iliyopita kujadiliana kuhusu masuala ya wanachama wao na hatua za kuchukuliwa dhidi ya wanaovunja Katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Yanga mtaa wa Twiga na Jangwani jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mohamed Msumi alisema wote wanaokiuka Katiba ni vema wakaitwa na kamati husika na kuhojiwa na taarifa zao zifike kwa uongozi na baadaye wapewe barua ya kufukuzwa uanachama.

“Ni haki ya kila mwanachama ambaye hakuridhika na jambo linalohusu katiba kuchukua hatua kwa kwenda kwenye vyombo vya juu kama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), lakini sio kutukanana wenyewe kwa wenyewe na kuvunja Katiba, ikiwa wapo waitwe wajieleze wamepata wapi mamlaka ya kukiuka taratibu, kama wametumwa na matawi waseme,”alisema.

Kauli hiyo ya Msumi imekuja siku chache baada ya baadhi ya wanachama wa Yanga kupeleka malalamiko TFF kuishtaki Yanga kwa kuvunja Katiba kwa kusogeza mbele uchaguzi mkuu, maamuzi yaliyopitishwa kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.

Msumi alisema Mwenyekiti wao Yusuf Manji hapaswi kulaumiwa kwa vile sio yeye aliyevunja Katiba isipokuwa wanachama wote waliokuwemo kwenye mkutano huo ambao walikubali kwa pamoja uchaguzi usogezwe mbele.

“Mkutano Mkuu ndio wenye mamlaka ya kumwongezea muda kiongozi wao, ndio maana hayo yote yalifanyika huko, sasa kama ni kuvunja Katiba wanachama ndio wenye makosa sio Manji,” alisema.

Alisema wanachama wote wanahitaji kushirikiana na kuwa kitu kimoja, lakini sio kuendeleza matusi na kuwapa faida Azam wazidi kupata mafanikio kwani ni maadui wao kimichezo.

“Haiwezekani udhaifu wetu na ubabe katika kutukanana utupelekee kuja kufanya vibaya katika klabu yetu, ni dhahiri kuwa tutawapa faida maadui zetu, mwisho wake tutazidi kuporomoka, watani zetu Simba watafurahia,”alisema.

KLABU ya Chelsea imemtangaza ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi