loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima Kagera washauriwa kupanda viazi vitamu

Ushauri huo ilitolewa jana na Germinus Nyeho kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Maruku wakati wa mafunzo kwa wakulima na maofisa ugani 60 kutoka Wilaya za Bukoba na Missenyi waliyoyapata juu ya uzalishaji wa mbegu bora za viazi.

Nyeho alisema wananchi wa mkoa wa Kagera wamekuwa na dhana kuwa zao la ndizi ndio zao pekee linaloweza kuliwa na kuwaongezea kipato, jambo ambalo amesema ni vyema wakatambua kuwa zao hilo kwa sasa limekumbwa na ugonjwa wa unyanjano na kufanya upatikanaji wake kuwa mgumu.

Aliongeza kuwa kama kituo chao cha utafiti waliamua kulichagua zao hilo na kuwashauri wananchi kulifanya zao mbadala pia lina virutubisho vingi ikiwemo kuongeza vitamin A, protini na kupunguza utapiamlo.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Angela Sebastian, Bukoba

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi