loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walimu kusomeshwa

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Jenista Mhagama alisema hayo juzi baada ya ziara yake ya kukagua miundombinu ya awamu ya kwanza ya mradi huo unaomalizika mwishoni mwa mwaka huu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

Alisema Benki ya Dunia, ambayo ni mfadhili mkuu wa mradi huo imeshakubali kufadhili awamu ya pili ya mradi na sasa wanaendelea na mchakato kuonesha ni kiasi gani cha pesa kinahitajika huku wakisaidia kuziba pengo la kuanguka kwa dola mwaka 2008 hali iliyosababisha baadhi ya miradi kutokamilika.

Alisema katika awamu ya kwanza ya mradi walikubaliana kupewa Dola za Marekani milioni 100 lakini zilipatikana milioni 90.

Alisema hata hivyo wamekubali kumalizia kiasi hicho cha fedha kilichokosekana kutokana na mtikisiko wa kiuchumi duniani kote wakati huo.

Mhagama alisema baada ya kushuhudia ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo maktaba, maabara na majengo pia mradi huo umewezesha kusomesha walimu na wakufunzi, kununua gari pamoja na vifaa vya kufundishia.

"Kutokana na kukamilika kwa mradi huu Watanzania wategemee mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu na kutoa ubora wa elimu na sasa tunakamilisha kuanza kwa awamu ya pili ya mradi huo ambapo pia tutasomesha walimu,” alisema Mhagama.

Mratibu wa Mradi huo Taifa, Dk Kenny Hosea alisema walimu na wakufunzi walipata mafunzo ya muda mrefu na mfupi na wanane walipata shahada za uzamili, 398 shahada za uzamivu katika vyuo bora duniani vya Uingereza na Australia na asilimia 30 wakisoma katika vyuo vikuu vya Afrika Kusini na Korea.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi