loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Walimu wa sayansi wahitajika Unguja, Pemba

Waziri wa Wizara hiyo, Ali Juma Shamuhuna aliyasema hayo wakati alipokutana na ujumbe wa Benki ya Dunia ikiongozwa na Mwakilishi wa taasisi hiyo nchini Pihillipe Dongier, mjini hapa.

Alisema lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa kupata wataalamu katika sekta hiyo.

Shamuhuna alisema licha ya misaada mingi inayotolewa na taasisi hiyo bado kiwango cha elimu hakijapiga hatua kubwa ya kuridhisha zaidi katika Sekta ya Sayansi ikiwemo huduma za maabara.

“Tunakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa walimu wa sayansi , waliopo sasa wametoka Nigeria na wanakaribia kumaliza muda wa mkataba wao,” alisema Waziri huyo.

Aidha Shamuhuna alichukua nafasi hiyo kuipongeza Benki ya Dunia kwa misaada yake katika sekta ya elimu ambayo imeleta mafanikio makubwa.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Dongier aliitaka Wizara hiyo kuorodhesha mahitaji yake yote katika kikao cha pamoja na watendaji wa benki hiyo.

“Benki ya Dunia kwa ujumla imefurahishwa na hatua kubwa iliyofikiwa katika kuimarisha elimu ambayo imetoa fursa kwa watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule kupata fursa hiyo,” alisema Mwakilishi huyo.

Benki hiyo imesaidia mradi mkubwa wa ujenzi wa shule za kisasa za sekondari 19 za Unguja na Pemba zikiwa na huduma muhimu ikiwamo maabara.

Mkuu wa wilaya na Arumeru Jerry ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi