loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Walimu wasifu fedha za rada kununua madaftari

Pongezi hizo zilitolewa na walimu wakuu wa shule za msingi kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na gazeti hili kuhusiana na utekelezwaji wa ahadi za serikali.

Shule zilizotoa pongezi hizo ni pamoja na Tutu, Kisiriri, Lulumba na Kizega. Akizungumza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tutu, Rebeca Madale alisema ni haki kwa ya shule husika kuipongeza serikali kwa kuwa walipata mgao wa vitabu vingi na ambavyo vimekuwa msaada wa kutosha kwa wanafunzi.

“Kwa kweli inatupasa kushukuru, tulivipata vitabu hivyo kwa awamu mbalimbali…ila tunaikumbusha serikali kuhusu vifaa na vitabu vya elimu ya awali ambavyo havikuwemo katika mgao huo,” alisema Rebeca.

Alisema pamoja na kuipongeza serikali, lakini pia wanazishauri halmashauri zinazohusika kugawa vitabu hivyo kushirikisha wadau ili kujua ni eneo lipi ambalo lina mapungufu zaidi kuliko kusambaza bila kujadili jambo ambalo linaweza kusababisha eneo moja kuwa na upungufu huku lingine likiwa limeongezewa kwa kiwango kikubwa.

Alisema kwa shule yake alipokea vitabu vya chenji ya rada mara nne huku akipokea vingine vilivyotolewa na serikali mara tatu ambavyo kwa pamoja vilikuwa vya masomo ya hisabati na sayansi ambavyo vilikuwa vingi huku vya uraia na Kiswahili vikiwa vichache.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisiriri, Gerson Mkoma alisema ahadi hiyo ya vitabu ilifika pamoja na miongozo na hata muhtasari ambavyo walivipokea kutoka Bohari ya Elimu.

Alisema karibu masomo yote kila mwanafunzi ana kitabu chake ikiwa kwa sasa ni takribani kama uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili tofauti na katika darasa la awali ambapo mwalimu pekee ndiye anayekuwa na kitabu.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Lulumba, Jacob Izack alisema vitabu hivyo vilifika na kupunguza tatizo la vitabu kwa kiasi kidogo kwani shule yake ina wanafunzi 410 ikilinganishwa na vitabu alivyopata.

Hata hivyo, alisema kwa madarasa ya juu kuanzia darasa la tatu hadi la saba uwiano wa vitabu shuleni kwake ni baadhi ya vitabu kutumiwa na wanafunzi wawili kwa kitabu kimoja huku masomo mengine yakiwa ni kitabu kimoja kwa wanafunzi wanne.

Serikali iliahidi kununua vitabu na madawati kutokana na fedha za malipo ya fidia ya rada na kuahidi kusambazwa katika halmashauri mbalimbali nchini kwa usawa.

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu, Kiomboi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi