loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walimu wasusia kikao wakitaka posho

Walimu hao ni kati ya walimu 200 kutoka wilaya tano za mkoa huo waliokuwa wakishiriki semina ya siku ya tano.

Wakizungumza katika viwanja vya Shule ya Sekondari Bariadi mjini hapa ambapo semina hiyo ilikuwa ikifanyikia, walimu hao walisema barua za mwaliko ziliwaeleza semina itakuwa ya siku 10, lakini walishangazwa kupunguzwa siku hizo na kubaki siku tano.

Walimu hao walibainisha kuwa wamekuwa wakiishi kwa shida bila kupata posho ya kujikimu tangu walipofika na kwamba walikuwa wanadaiwa fedha na wahudumu wa nyumba za kulala wageni.

Ofisa Elimu Mkoa, Aloyce Kamamba alisema kuchelewa kwa malipo kutokana na kuchelewa kwa mhasibu kutoka katika Wizara ya Elimu ambaye ndiye alitakiwa kuwalipa.

Semina hiyo mahsusi kwa walimu wa sayansi inayofanyika kote nchini, inaendeshwa na Wizara ya Elimu kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi walimu wa masomo hayo.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Baridi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi