loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wambura kukaangwa tena

Wambura amekata rufani kwa kamati hiyo baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba kumuengua kuwania nafasi hiyo kwa madai alikiuka kanuni za uchaguzi kwa kufanya kampeni kabla ya muda, licha ya kuwa alikwishaonywa kufanya hivyo kwa maandishi.

Awali, Wambura na mgombea mwenzake wa nafasi hiyo Evance Aveva walidaiwa kufanya kampeni katika zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kugombea, ambapo walipewa onyo kali kwa maandishi wakitakiwa kutorudia tena kitendo hicho.

Kutokana na kuenguliwa huko, Wambura alisema hatokubaliana na uamuzi huo hivyo, juzi aliwasilisha barua yake ya rufani TFF ili kupata haki yake ya kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Habari za uhakika zilizopatikana ndani ya TFF jana, zinasema kikao hicho kitakutana leo kuanzia saa nane mchana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba Dk Damas Ndumbaro amealikwa.

Hii ni mara ya pili kwa Wambura kukata rufaa kwenye kamati hiyo, mara ya kwanza alikata kupinga kuenguliwa kwenye uchaguzi akidaiwa si mwanachama halali, ambapo kamati hiyo ya rufani chini ya Julius Lugaziya ilimrejesha na kusema kuwa Wambura ni mwanachama halali wa Simba.

Uchaguzi wa Simba umepangwa kufanyika Juni 29.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi