loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wambura, wenzake 71 wafukuzwa Simba

Uamuzi huo umewakumba pia wanachama 71 walioguswa na kosa hilo baada ya kuipeleka Simba mahakamani katika fukuto la Uchaguzi Mkuu uliofanyika Juni 29, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo umechukuliwa jana kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam ambako pia walipitisha maamuzi mbalimbali ya Katiba yao, katika zoezi lililosimamiwa na mwanasheria Damas Ndumbaro.

Mkutano huo uliokuwa ukiendeshwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva baada ya kufika ajenda ya kuwajadili wanachama hao akiwamo Wambura, alisema kabla ya kufikisha suala hilo kwa wanachama, alifanya juhudi kubwa kukutana na wanachama hao, jambo ambalo walionesha kuliwekea ngumu.

“Nikiwa kama rais nilifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wanachama hawa wanafuta kesi yao mahakamani, lakini waligoma, sambamba na kukataa kikao cha usuluhishi dhidi yao.

“Hii ilinifanya mimi na Kamati yangu ya Utendaji ifikishe suala hilo katika Mkutano Mkuu ambao kwa kawaida ndio wenye klabu yao,” alisema Aveva aliyeingia madarakani Juni 29, mwaka huu.

Hata hivyo, wakati Aveva anazungumzia jambo hilo, kelele zilikuwa zinapigwa ukumbi mzima na wanachama zaidi ya 860 waliohudhuria mkutano huo, kuwa hakuna haja ya kuwajadili zaidi ya kuwafukuza kwa kuvunja Katiba ya Simba.

Licha ya kelele hizo, kura zilitumika ambapo wote waliinua mikono juu kutaka wanachama hao kwa pamoja wafukuzwe uanachama. Wambura anadaiwa kuipeleka Simba mahakamani mwaka 2010 wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu, wakati wengine 71 walifungua kesi baada ya kuwapo kwa mzozo wa uchaguzi wa mwaka huu.

Alipoulizwa kuhusu uamuzi huo, Wambura aliyewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Simba, alisema jana ni Jumapili, anapumzika hawezi kuzungumzia suala lolote.

Kabla ya uamuzi huo kuchukuliwa, wanachama wa klabu hiyo walipata fursa ya kupitisha maamuzi mbalimbali ya Katiba yao, chini ya mwanasheria wao Damas Ndumbaro.

Vipengele vilivyopitishwa ni vinavyohusu uundwaji wa Baraza la Wadhamini, Baraza la Wazee na wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa kuteuliwa ambapo sasa hawataguswa na vigezo kama walivyokuwa wajumbe wa kuchaguliwa.

Katika mkutano huo uliokuwa na ajenda 14 ambazo zote kwa pamoja zilipita. Katika hatua nyingine, mkutano huo pia umepitisha Bajeti ya Sh 3,008,600,000, wakati makusanyo yao kwa mwaka wa fedha 2014 na 2015 yatafikia Sh 2,681,000,000.00.

Makusanyo hayo yatatokana na fedha mbalimbali kutoka kwenye vyanzo vyao vya mapato, ikiwamo fedha za viingilio, kodi ya majengo, ada ya uanachama, mikataba ya wadhamini wao, wakiwamo TBL, Azam TV na mingineyo.

Aidha, Aveva pia aliwaambia wanachama kuwa uongozi uliomaliza muda wake wa Ismail Aden Rage, haujaacha kitu zaidi ya madeni yaliyofikia Sh milioni 327 kwa kipindi cha uongozi wake.

Mkutano wa Simba umefanyika jana ikiwa ni kuelekea kwenye Simba Day, ambapo kilele chake ni Agosti 9, mwaka huu, ambayo timu yao hiyo itaingia uwanjani kumenyana na Zesco ya Zambia.

BERNARD Morrison ameng’ara baada ya kuifungia timu yake mabao mawili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi