loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wamiliki wa nyumba walipe kikamilifu kodi ya majengo

Kodi hiyo ni moja ya maeneo sita, ambayo yamepewa kipaumbele katika suala la ukusanyaji wa kodi. Kodi hiyo ya majengo, imerejeshwa hivi karibuni na serikali kuu kwa serikali za mitaa nchini.

Tunaunga mkono hatua hiyo ya Waziri wa Fedha, kwa sababu tunajua alilenga kupata picha halisi ya kinachoendelea katika mkoa huo. Pia, alitaka kuelewa changamoto zinazowakabili watendaji wa manispaa zote tatu za Ilala, Kinondoni na Temeke.

Tunajua kuwa Serikali Kuu imerudisha jukumu la kukusanya kodi ya majengo kwenye serikali za mitaa, kwa sababu ni rahisi kwa serikali hizo kukusanya kodi hizo kuliko serikali kuu.

Sababu nyingine ni kuwa viongozi wa serikali za mitaa, wanajua nyumba zote zilizopo kwenye maeneo yao kuliko viongozi wa serikali kuu.

Hali kadhalika, tunaipongeza serikali kurejesha kodi hiyo ya majengo kwa serikali za mitaa, kwa sababu kodi hizo zimekuwa kilio cha muda mrefu cha halmashauri za majiji, manispaa na wilaya nchini.

Kwa Dar es Salaam, kodi ya majengo ilikuwa inategemewa mno na Halmashauri ya Jiji na halmashauri za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni, kabla chanzo hicho hakijachukuliwa na serikali kuu miaka ya karibuni.

Kodi hiyo ina umuhimu mkubwa na ni moja ya vyanzo vikubwa vinavyotegemewa. Ndiyo maana mwaka 2013 Serikali kuu iliamua kuwa kodi hiyo ni ya mfano katika mpango wake wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Tuna imani sasa halmashauri hizo za Dar es Salaam, zitaongeza maradufu ukusanyaji wa kodi hiyo, ili kuongeza mapato ya serikali, yanayotumika katika kutoa huduma za jamii na kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Nia imani yetu kuwa halmashauri hizo za Dar, zitashirikiana na viongozi wa kata na mitaa, kutambua na kuorodhesha majengo yote, yaliyokuwa yakilipa kodi ya majengo huko nyuma na pia kutambua mengine mapya, ambayo yamejengwa karibuni.

Majengo yote jijini yanatakiwa kuthaminiwa haraka. Kuna majengo zaidi ya 20,000 jijini, ambayo yanaweza kuzipatia halmashauri hizo mabilioni ya shilingi, ikiwa ni kodi ya majengo.

Kuna umuhimu wa halmashauri hizo, kutumia viongozi wa mitaa na kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na vipaza sauti, kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu kulipa kodi hiyo ya majengo kwa maendeleo na uchumi wa Taifa.

Kwa watu binafsi tunaomba waone umuhimu wa kulipa kodi hizo kwa hiari. Waache kuficha majina ya wamiliki halisi wa majengo na wasisubiri kusukumwa na vyombo vya dola. Tunashauri halmashauri hizo, zitumie njia ya picha, kuwabaini wanaokwepa kulipa kodi hiyo.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi