loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafamilia washitakiana,wagombea maiti ya daktari

Mgogoro huo baina ya mke mdogo na ukoo wa Dk Senga, umechukua sura mpya baada ya juzi kutolewa amri ya mahakama kufukuliwa mwili wa Senga aliyefariki Novemba 7 mwaka huu na kuzikwa na mke mdogo akisaidiwa na mwanawe wa kiume, bila makubaliano na familia ya marehemu.

Akizungumza na mwandishi wa habari, mdogo wa marehemu, Dominick Senga (67) alisema kaka yake alioa mke wa ndoa, wakaachana, baadae akaoa mke wa pili naye waliachana, tena mke huyo wa pili aliolewa na mwanamume mwingine aliyefunga naye ndoa ambayo haikudumu wakatengana, akiwa na mtoto wa kiume wa marehemu.

lisema wakati Senga alipostaafu kazi ya udaktari, alijenga nyumba Chanji na kufungua duka la dawa akawa anaishi na baadhi ya watoto wa mke mkubwa, ambaye naye alikuwa ameshaolewa na mume mwingine na kuwaacha watoto kwa baba yao.

Alisema Senga alianza kuumwa miezi mitatu iliyopita, ndipo wiki tatu zilizopita alifika Chanji kwa mtoto wa mke mdogo aliyekuwa ameolewa Bangwe na kuachika, akamuomba baba yake waende kunywa supu na huko ndiko alikofikwa na mauti.

Alisema tangu daktari huyo afariki Novemba 7, wanafamilia hao wamekuwa wakivutana, ambapo mke mdogo wa marehemu na mtoto wake wa kiume wanataka wao wamzike marehemu, kwa madai kuwa walikuwa wakimuuguza.

Lakini, alisema wadogo zake daktari, wanandugu na familia ya mke mkubwa wataka ukoo ukamzike marehemu kwa taratibu za kiukoo. Mvutano huo uliwafikisha wanandugu mahakamani, kuomba msaada wa kisheria juu ya nani mwenye haki ya kumzika marehemu.

Lakini, wakiwa mahakamani hapo, mke mdogo wa marehemu na mwanawe, Cosmas Senga waliuchukua mwili chumba cha maiti na kwenda kuuzika katika makaburi ya Mandela mjini hapa.

Ndugu walimweleza hakimu Rosario Mugisa kuwa, upande wa pili wametoka kuzika ndipo hakimu alitoa amri ya kuufukua mwili na kuuhifadhi chumba cha maiti mpaka hapo mahakama itakapotoa uamuzi juu ya nani anapaswa kumzika Dk Senga.

Hata hivyo, kazi ya kufukua mwili haikufanikiwa jana, kwani cheti cha kifo kilikuwa hakijapatikana na jitihada za walalamikaji kutafuta cheti hicho, zinaendelea.

UDANGANYIFU wa kitaaluma ambao hujikita katika aina nyingi na nyanja ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi