loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi vyuo vya Ualimu wafundwa

Mwito huo ulitolewa hivi karibuni na mke wa Rais, Mama Salma Kikwete wakati akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Chuo cha Ualimu Nachingwea baada ya kumalizika kwa futari aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi wa wilaya iliyofanyika chuoni hapo.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa kupitia Wilaya ya Lindi Mjini, alisema si jambo jema kwa Mwalimu kuvaa mavazi yanayoonesha sehemu za miili yao ikiwemo kata mikono, nguo zinazobana na sketi fupi na kwamba kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na haiba ya Ualimu.

Alisema, “Siku hizi kuna baadhi ya watu wanavaa mavazi yasiyoendana na utamaduni wa Mtanzania, ninyi kama walimu ambao ni kioo cha jamii na mnawafundisha wanafunzi madarasani msifanye hivyo kwa kufanya hivyo watoto wataiga na kufikiria kuwa kuvaa mavazi hayo ni sawa.”

Alitaka wanafunzi hao kutochagua maeneo ya kwenda kufanya kazi wamalizapo masomo yao na kupangiwa vituo vipya vya kazi kwani kazi ya Ualimu ni wito na kama mtu hakuipenda kazi basi angechagua fani nyingine za kusoma.

“Baadhi ya walimu wamekuwa wakikataa kwenda kufanya kazi katika maeneo ya vijijini, na wengine wakipangiwa vituo vya mbali na mjini wanaogopa na kudiriki hata kuacha kazi, kama ni hivyo kwa nini ulipoteza fedha na muda wako kusomea Ualimu?” Alihoji.

Mama Kikwete ambaye kitaaluma ni Mwalimu , alisoma kwenye Chuo hicho cha Nachingwea. Akiwa chuoni hapo, alitembelea bweni la wasichana la Kawawa ambako alikuwa akilala.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Anna Nkinda - Maelezo, Nachingwea

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi