loader
Picha

Wanahabari wajitathimini

Kitaifa, maadhimisho haya yanafanyika mkoani Dodoma. Ikumbukwe kuwa miongoni mwa kazi za vyombo vya habari, ni kuelimisha, kutoa taarifa, kuburudisha, kukosoa na kuchochea maendeleo ya watu.

Ili kutimiza azima hiyo, vyombo vya habari vinazo kanuni za maadili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vinazingatia weledi hasa kwa kusema ukweli wenye manufaa kwa jamii, kufichua uhalifu na kupaza sauti za wanyonge ili viendelee kuwa sauti ya wasio na sauti.

Wakati wanahabari wakiendelea kutafakari maadhimisho haya, wajiulize kila mmoja kwa nafasi yake au kwa kila taasisi kuwa, ni kwa kiasi gani wamechangia kuleta hofu kwa jamii, badala ya kuleta tumaini kutokana na habari wanazoandika au kutangaza.

Wajiulize ni kwa kiasi gani kabla ya kuandika au kutangaza habari, wameifanyia uchunguzi wa kina na kujiridhisha kitaaluma kuwa, habari wanayoitangaza, haishushi utu wa mtu na itajenga na kuisaidia jamii.

Tunasema, kwa muktadha huo kuwa, ni wajibu na haki ya wanahabari kuhakikisha wanakuwa daraja na kiunganishi cha wanajamii na viongozi kupata maoni mbalimbali toka pande zote na kufikisha pande nyingine.

Kwa msingi huo, tunatarajia katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na teknolojia hasa katika habari na mawasiliano (ICT), wanahabari wanazingatia weledi na hivyo, kujitofautisha kimaudhui na kiutalaamu dhidi ya uandishi wa mitandao ya kijamii unaofanywa na yeyote bila kuzingatia utu wala maadili ya taaluma ya habari.

Miongoni mwa yanayodhihirisha mitandao hiyo kutotimiza wajibu wake na kuzingatia utu, ni pamoja na baadhi ya wanahabari (vyombo) kutaja majina halisi au kuchapisha picha zenye sura wazi za waathirika wa uhalifu ukiwamo ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.

Mengine ni pamoja na uchapishaji picha za kutisha na habari zinazochochea hisia za kimwili huku nyingine, zikilenga biashara badala ya maendeleo ya watu.

Ndiyo maana tunasema, maadhimisho haya hayana budi kutufanya tujitafakari kuwa, taarifa na kazi zetu zinalinda utu wa mwanadamu? Je, zinalinda maadili ya Mtanzania na Mwafrika kwa jumla?

Je, kazi tunazozifanya zinalinda utamaduni wa uhai, au zinachochea utamaduni wa kifo?

Tujiulize, katika kazi zetu tunatumikia umma, au tunatumikia nafsi zetu na kuwatumikia wahalifu kwa nguvu za pesa.

Ndiyo maana tunasema, kalamu au vyombo vyetu vitumike kuunganisha umma, kujenga amani, usalama na mshikamano; pamoja na kuhakikisha tunaisadia serikali na watu wake (wananchi) kulinda utamaduni na usalama wa nchi.

MOJA ya vitu ambavyo vinaelezwa kuwa huenda vikaibua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi