loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wananchi kufundishwa fursa sekta ya madini

Lengo la mafunzo hayo yanayoendeshwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ni kuwezesha wananchi kutumia fursa hizo kuinua kipato chao na taifa kwa ujumla.

Makubaliano hayo yalifikiwa hivi karibuni jijini Mwanza wakati wa mkutano ulioandaliwa na Idara ya Madini kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja baina yake na kampuni za madini katika kutekeleza Sera ya Madini ya mwaka 2009.

Wajumbe wa mkutano huo, walipitisha maazimio yanayolenga kuhakikisha Watanzania wanashirikishwa ipasavyo katika Sekta ya Madini. Miongoni mwa maazimio, ni ya kujenga uelewa kwa wananchi watambue fursa zilizopo na kuzitumia.

Pia walikubaliana ufanyike utafiti utakaoainisha mianya iliyopo katika utoaji huduma hususan maeneo ambayo wananchi wanaweza kutoa huduma kwa kampuni za madini wafanye hivyo.

Akifafanua, Kamishna wa Madini, Ally Samaje alisema wananchi wana haki kutoa huduma zilizo ndani ya uwezo wao.

Alisema Serikali itahakikisha haki hiyo inatekelezwa kama inavyostahili.

“Sisi kama Serikali tunataka kuboresha ushirikishwaji wazawa katika Sekta ya Madini na ni lazima kampuni za madini zihakikishe wazawa wanashirikishwa ipasavyo,” alisisitiza.

Aidha, maazimio mengine yaliyofikiwa katika mkutano huo ni Serikali kwa kushirikiana na kampuni, kujengea wazawa uwezo kwa kutilia mkazo Sekta ya Kilimo na Uzalishaji.

Vilevile, pande hizo mbili zilikubaliana kwamba, kwa kuwa ushirikishwaji wazawa ni suala la kisera, iko haja ya kufanyia marekebisho sheria na kanuni za madini kuhusu ushirikishwaji wa wazawa ili kuhakikisha wazawa wanapata haki stahiki.

Pia, iliafikiwa kuwa kuanzishwe Kamati Maalumu itakayoshughulikia masuala ya ushirikishwaji wazawa katika Sekta ya Madini ambayo pamoja na mambo mengine itaainisha mahitaji na viwango katika eneo husika katika hali ambayo ni shirikishi, na pia kusaidia kuainisha fursa zilizopo katika sekta.

Wajumbe wa mkutano huo pia walikubaliana kuwa Wizara ya Nishati na Madini iandae mkutano wa kila mwaka kujadili suala la ushirikishwaji wazawa ambao utashirikisha kampuni zote za madini, wafanyabiashara na wazalishaji wazawa, jamii zinazozunguka migodi pamoja na wizara na taasisi nyingine za serikali zinazohusika.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Veronica Simba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi