loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaoingiza bidhaa bila kulipa ushuru kukiona

Aidha, ameeleza kuwa pamoja na suala hilo pia watafanya utafiti kuangalia soko la betri na kiasi zinazoingia na zinazolipiwa ushuru na ikibainika kuwepo zinazoingia bila kulipiwa ushuru watachukua hatua.

Chiza alisema hatua hizo na nyingine watazifanya kupitia Baraza la Taifa la Biashara kwa kuunda kamati maalumu na kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mamlaka ya Mapato (TRA) na taasisi nyinginezo.

“Katika utafiti huu pia, tutaangazlia mazingira ya biashara, ikiwa ni pamoja na ulipaji kodi wao kwani asilimia 98 ya malighafi ya bidhaa hii inaingizwa kutoka nje ubora wa bidhaa pamoja na uzalishaji wa bidhaa hizo nchini China,” alisema.

Waziri alisema hayo baada ya kufanya ziara kutembelea kiwanda hicho kilichoanza uwekezaji tangu mwaka 1968 lakini uzalishaji wake umezidi kushuka kutokana na sababu mbalimbali ambapo sasa wanazalisha betri 250,000 kwa siku badala ya zaidi ya milioni moja walizokuwa wakizalisha.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Yoshiyuki Sako alisema wana changamoto katika soko kutokana na betri kutoka nchini china kuuzwa kwa bei nafuu ya Sh 300 wakati betri zao wanauza kwa Sh 500.

Naye, Meneja Masoko wa kiwanda hicho alisema walifanya utafiti na kugundua gharama za kutoa betri nchini China, kodi na mengineyo ni Sh 350 hadi 400 lakini alishangazwa na kuona zinauzwa kwa bei ya chini, kuwepo kwa bidhaa hizo zisizo na nembo ya TBS na mengineyo.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi