loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaojiandikisha waongezeka

Baadhi ya wananchi walidai ongezeko hilo linatokana na wananchi wengi kudharau kujiandikisha mapema.

Akizungumza na gazeti hili, mkazi wa Mtoni aliyejitambulisha kwa jina la Said Mzee alipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kuagiza kufunguliwa mapema kwa vituo hivyo, lakini kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya watendaji na mashine katika vituo ili kuhudumia idadi kubwa ya watu.

Alisema watu wanazidi kuongezeka kutokana na wengi wao wakati uandikishaji unaanza, hawakujitokeza kwa kusubiri siku za mwishoni, hali inayochangia foleni kubwa ya watu vituoni.

“Kwa mfano mimi mwenyewe nilikuwa sipo, kwa hiyo nilitegemea nikirudi nitakuta watu wamepungua vituoni lakini ndiyo idadi inaongezeka kila siku. Lakini tunashukuru tume imeona umuhimu wa watu wote kuandikishwa,” alisema Mzee.

Katika kituo hicho kilichopo mtaa wa Mfenisini Kata ya Chamazi, baadhi ya wananchi wamejikuta wakifika vituoni hapo usiku wa manane ili waweze kupata nafasi ya kujiandikisha.

Idadi hiyo imekuwa ikiongezeka huku Tume ikiongeza mashine, waandikishaji na watendaji katika baadhi ya vituo ili kuhakikisha hakuna mwananchi atakayeachwa bila kuandikisha. Katika baadhi ya vituo katika maeneo ya Kisutu, Mnazi Mmoja na maeneo ya katikati ya jiji, idadi ya watu ilikuwa ni chache zaidi.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi