loader
Picha

Wanaosamehewa kodi kutangazwa

“Sambamba na kupunguza misamaha ya kodi na kuongeza haki na usawa katika kutoa misamaha, kuanzia mwaka 2014/15 serikali itachukua hatua kuu mbili muhimu”, alisema.

Saada alisema hatua ya kwanza itakayochukuliwa ni Serikali itakuwa inatoa taarifa ya misamaha ya kodi kila robo mwaka, kwa kuwatangaza walionufaika na misamaha kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha.

Taarifa hiyo itajumuisha majina ya watu, taasisi, asasi na kampuni zilizonufaika na misamaha ya kodi, thamani na sheria iliyotumika kutoa misamaha hiyo.

Alieleza kuwa zoezi hilo, litahusisha taarifa ya misamaha ya kodi ya kuanzia mwaka 2010 na kuendelea.

“Hatua hii itasaidia kuleta uwazi na uwajibikaji katika suala la misamaha ya kodi na kuwafanya wananchi wajue ni nani anayenufaika na misamaha hiyo,” alisema.

Alisema, hatua ya pili itakayochukuliwa ni kutoa taarifa ya kina ya misamaha yote ya kodi iliyotolewa na kuiwasilisha bungeni kila mwaka ili wabunge wapate nafasi ya kujadili na kutoa maoni yao.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Nelson Goima, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi