loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Wanawake Afrika fuatilieni maendeleo ya wasichana’

Alisema hayo Dar es Salaam katika hafla ya wenza wa mabalozi nchini, waliokutana na mke wa Rais, Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya 2015.

Mama Mpango alisema katika kuyafikia maendeleo ya nchi, ni vyema wote wanaume na wanawake wakashiriki kwa pamoja na kwa jitihada ambazo baadae kila mmoja atanufaika na matunda hayo.

Alisema wanawake wanatakiwa kuhamasisha watoto wao wa kike, kuzingatia masomo kama wanavyofanya kwa wanaume na kamwe isitokee mmoja kuachwa nyuma kwa kigezo cha kuwa mtoto wa kike.

“Dunia ya sasa ni ya utandawazi ambao kukua kwa maendeleo hakuangalii mtoto wa kike ama wa kiume hivyo ni vyema wote wakahamasishwa kwenda shule na kuzingatia masomo na sio mmojawapo kuachwa kwa kuwa ni mtoto wa kike,” alisema Mama Mpango.

Kuhusu Mama Salma, alisema amekuwa na nguvu kubwa ya kutafuta kuwakomboa wanawake na kuwawezesha kuiuchumi, kielimu na hata kiafya.

TANZANIA na Burundi zimetiliana saini makubaliano katika ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi