loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake `makuli’ wa Kiarabu Morocco

Ni asubuhi na mapema , na jua limechomoza katika eneo la Melila ambalo ni sehemu ya mpaka kati ya Morocco na Uhispania, huku vumbi likionekana na shughuli zikiendelea za kutayarisha mizigo tayari kuivusha mpaka.

Mizigo hiyo inajumuisha nguo za mitumba, vitambaa , vifaa vya kutumia kwenye bafu na choo vyote vikiwa vinakwenda katika masoko ya Morocco na kwingineko.

Maelfu ya watu wako hapa na kelele ni nyingi kupita kiasi. Mizigo mikubwa yote ikiwa imefungwa kwa vitambaa na kamba ndiyo inaonekana hapa kwa wingi. Na kando ya mizigo hiyo ni wanawake wa Morocco wenye kufanya kazi ya 'nyumbu'....kubeba mizigo hiyo.

Kazi hii wanaifanya kila siku katika eneo la Barrio Chino - mpaka wa kutoka Melila na kuingia nchini Morocco kwa wasafiri wa miguu pekee.

Ikiwa wanawake hawa watabeba mizigo hiyo basi inatajwa kuwa mizigo ya kibinafsi na kwa hivyo hawatozwi kodi.

Wanawake hao wana haki ya kuzuru Melilla kwa sababu wanaishi katika Mkoa wa Nador nchini Morocco. Lakini hawaruhusiwi kuishi katika eneo hilo linalomilikiwa na Uhispania.

Mwanamke mmoja kwa jina Latifa anapanga foleni yenye mamia ya wanawake wanaosubiri kuvuka ili naye apate muda wake wa kupita mpakani. Amekuwa akiifanya kazi hii kwa miaka 24 na analipwa dola nne (Sh 6,400) kwa kubeba mzigo huo na kuuvusha kuingia Morocco. Sio kazi anayopenda kuifanya.

"Nina familia ambayo lazima ilishwe,” anasema Latifa, “Nina watoto wanne wala sina mume wa kunisaidia-nilitalakiana naye kwa sababu alizoea kunipiga,” anasema Latifa. Wengi wa wanawake wanaofanya kazi hii kama Latifa, ni wanawake waliotalikiana na waume zao ambao lazima walishe familia zao.

Maisha ni magumu lakini katika jamii ya kitamaduni ya Morocco , hii ndio kazi pekee wanayoweza kufanya. Baadhi yao wanafanya safari mara mbili, tatu au nne kwa siku moja wakiwa wamebeba mizigo hiyo ya hadi kilo 80.

Malipo hapa yanatofautiana na wanawake hawa wanalalamika kuwa wakati mwingine wanalazimika kutoa rushwa kwa walinzi ili wawaruhusu kupita. Katika eneo la Melila kuna mjadala kuhusu ikiwa biashara hii kama ilivyo inapaswa kuendelea au la.

“MTU niliyefanya naye mahojiano alikuwa anafanya kazi kwenye ...

foto
Mwandishi: MELILA, Morocco

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi