loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Waomba sheria kurekebishwa kuwabana wadhalilishaji

Sheha wa kijiji cha Mzuri Makunduchi, Mwanabaraka Chimbeni Kheri alisema matukio ya ubakaji yamekuwa yakijitokeza kwa wingi katika kijiji hicho lakini kwa bahati mbaya hakuna watu waliotiwa hatiani.

Kwa mfano alisema katika shehia yake, watu wanne walituhumiwa kubaka katika mwaka 2003, lakini waliachiwa huru na mahakama kwa madai kwamba ushahidi haukujitosheleza wa kuweza kuwatia hatiani.

“Wazazi na wananchi kwa ujumla hivi sasa wamekata tamaa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kuhusu matukio ya ubakaji kwa sababu hakuna mtu anayetiwa hatiani na kwenda jela,” alisema.

Mratibu wa Shehia ya Mzuri ya wanawake na watoto, Zawadi Hamdu Vuai aliitaka Serikali kuifanyia marekebisho sheria ya ushahidi pamoja na makosa ya jinai ili kuwatia hatiani wahusika.

Mkazi wa Makunduchi Tasani ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema mtoto wake alibakwa na mwalimu wa shule ambaye aliachiwa na mahakama kwa ukosefu wa ushahidi alisema amesikitishwa na udhaifu wa sheria zilizopo ambazo hazitoi nafasi kwa wabakaji kutiwa hatiani.

Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha ya Sheria, Jaji Bakari Mshibe alisema tume yake tayari imezifanyia kazi sheria nne ambazo zinahitaji marekebisho.

Aliitaja Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nambari 7 ya mwaka 2004 pamoja na sheria ya ushahidi namba 5 ya mwaka 1917 zipo katika mchakato wa kufanyiwa marekebisho kwa sababu zimepitwa na wakati.

Mkuu wa Wilaya, Gift Msuya kwa niaba ya Mkuu ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi