loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wapongezwa kuwezesha bei ya mawasiliano kushuka

Profesa Mwandosya alitoa pongezi hizo juzi wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi zinazohusika na masuala ya udhibiti wa huduma mbalimbali kwa lengo la kujionea namna zinavyofanya kazi kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Miongoni wa taasisi alizozitembelea na anazotarajia kuzitembelea waziri huyo ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu(Sumatra), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA) Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alisema kimsingi tangu kuanzishwa kwa TCRA imefanya kazi kubwa na nzuri katika kuwahudumia wananchi katika nyanja ya mawasiliano na kudai mfano mzuri ni namna ambavyo gharama za mawasiliano zilivyo hivi sasa tofauti na hapo awali hatua inayotoa fursa kwa wananchi wengi kufanya mawasiliano.

Aidha alisema ziara yake katika taasisi hizo imelenga kuzijengea ushirikiano sanjari na kuzifanyia tathmini ya utendaji wa kazi zake akilinganisha na taasisi kama hizo katika nchi za Uganda na Kenya baada ya hivi karibuni kufanya ziara yake katika nchi hizo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma pamoja na mambo mengine kuhusu maendeleo ya mamlaka hiyo, alimshukuru Profesa Mwandosya kwa jitihada za kuwezesha mamlaka hiyo kufika mahali ilipo sasa.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimekubaliwa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi