loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wasanii kufanya onesho la wazi

Wasanii watakaoshiriki onesho hilo lijulikanalo kama Good Time ya ukweli na Coca Cola ni pamoja na Madee,Vanessa Mdee,Joe Makini na Diamond.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Meneja wa Bidhaa wa Coca-Cola waandaaji wa onesho hilo, Mourice Njowoka alisema onesho hilo ni la kwanza litakalofuatiwa na maonesho mengine ya bure mikoani.

Alisema Februari 22 itakuwa zamu ya mkoa wa Mwanza ambapo Diamond, TMK Wanaume Family pamoja na Madee watakuwa jukwaani.

Machi mosi itakuwa zamu ya Arusha ambapo onesho litafanyika katika uwanja wa Soweto na wasanii Jambo Squad, Vanessa Mdee na Joe Makini watatoa burudani.

Aliongeza kuwa Machi 8 jijini Mbeya litafanyika onesho katika Viwanja vya CCM Ilomba ambapo Madee na TMK Wanaume Family watatumbuiza.

Machi 15, onesho litafanyika katika kiwanja cha Majengo, Moshi na wasanii watakaopanda jukwaani ni pamoja na Diamond,Joe Makini na Jambo Squad Njowoka.

Alisema lengo kubwa la maonesho hayo ni kuwaweka karibu wananchi na kufurahia burudani kutoka kwa wasanii wao.

“Najua kuwa hawa wasanii wanapendwa na washabiki ambao wengi hawana fedha za kulipia kuona shoo, sasa tunawapatia fursa ya kuwaona bure kabisa,”alisema Njowoka.

Aliongeza kuwa wasanii itakuwa ni fursa kwao kuwa karibu zaidi na wapenzi wao wa burudani.

MSANII wa Kizazi Kipya, Beka Flavour ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi