loader
Picha

Wasanii, uongozi Bunge Maalumu wakutana

Hayo yalisemwa na mwanamuziki John Kitime kutoka Mtandao wa Wanamuziki Tanzania mjini alipozungumza na waandishi wa habari jana kuhusu ujio wao katika Bunge Maalumu.

Pamoja na kusema kwamba wasanii hao wako Dodoma kwa ajili ya kukutana na wajumbe wa Bunge la Katiba ikiwa ni mara ya tatu kufika tangu Bunge la Katiba lilipoanza, alisema ombi lao la pili ni milikibunifu itajwe rasmi kama moja ya aina za mali zinazohitaji kulindwa katika Katiba.

“Sababu ya kutaka kutambuliwa huku wasanii ni kundi kubwa kuliko hata baadhi ya makundi,” alisema na kuongeza kuwa wasanii wamekuwa wakifanya kazi kubwa lakini wamekuwa masikini kutokana na kutofaidika na kazi zao kwani hata nyimbo nyingi zinazopigwa redioni wasanii wamekuwa hawanufaiki na chochote na sasa wakati umefika kufaidika na kazi zao.

“Tulikuja na mapendekezo ya namna ya kuingiza hoja hizi zilizosahauliwa, mapendekezo yetu ni kuwa katika ibara ya 30 iongezwe aya moja tu na ibara ya 37 inayoongelea haki ya ulinzi wa mali itambue kuwa pamoja na mali zinazohamishika na zisizohamishika pia kuna mali isiyoshikika”.

Alisema wamezunguka katika kamati tisa kwa siku mbili na kukumbusha mapendekezo yao ambayo hayabebi tu wasanii bali wavumbuzi wa kiteknolojia, kibaiolojia, wasomi, watafiti na wananchi kwa ujumla.

Alisema mashirikisho ya sanaa yanawawakilishi kwenye bunge hilo ambaye ni Paulynus Mtenda ambaye amewahakikishia kuwa yote aliyowakilisha yamepokelewa.

Alipohojiwa wasanii watafanya nini iwapo mapendekezo yao hayataingizwa kwenye Katiba mpya alisema Katiba baada ya kujadiliwa bungeni itarudi kwa wananchi na kama mapendekezo yao hayatakuwepo watapiga kura kuikataa Katiba hiyo.

Kitime alisema kwamba Mwenyekiti wa Bunge hilo Samweli Sitta aliwapokea na kuwawezesha kukutana na kamati mbalimbali na kukumbusha mapendekezo yao kama wasanii katika Katiba ijayo.

Wakati huo huo wasanii nchini wametaka wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurudi bungeni ili kukamilisha kazi waliyoianza ili nchi ipate katiba yenye maslahi kwa miaka 50 ijayo.

Katika Mkutano na waandishi wa habari jana Mjini hapa Simon Mwakifamba kutoka Shirikisho la Wasanii Tanzania (TAFF) alisema ni vyema Ukawa wakarudi bungeni ili kukamilisha kazi waliyoianza.

NBA iko kwenye mazungumzo ya kuanza tena msimu kwenye hoteli ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi