loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasanii wajipanga kumuenzi Kanumba

Kanumba alifariki miaka miwili iliyopita na ili kuenzi mchango wake kwenye tasnia ya filamu nchini, familia yake imeanzisha mfuko wa Kanumba the Great Foundation kwa lengo la kuendeleza yale aliyokuwa akiyapenda.

Mfuko huo utazinduliwa Jumatatu ijayo kwenye ukumbi wa Dar Live, zitakakofanyika sherehe za kumbukumbu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, rais wa Shirikisho la wasanii Tanzania Simon Mwakifamba alisema moja ya kazi iliyokuwa ikifanywa na Kanumba ni kuibua vipaji vipya na kuwapa mafunzo wasanii chipukizi.

“Kutokana na kutambua mchango wake tutaungana kwa pamoja katika kumuenzi kwa kutembelea kituo cha watoto yatima Sinza siku ya Jumapili na kutoa kile tulichonacho,” alisema.

Alisema Aprili 7, mwaka huu watafanya ibada kwenye Kanisa la Kilutheri Kimara Temboni na baadaye watakwenda katika kaburi la Kanumba na kuweka mashada ya maua kisha jioni wataungana katika tamasha la uzinduzi wa Taasisi ya Kanumba kwenye ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Mwakifamba alisema kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Snura, Chege na Juma Nature na kwa upande wa bendi kutakuwa na kundi la taarab la Jahazi na bendi ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Kuhusu viingilio, Mwakifamba alisema vitakuwa Sh 2,000 kwa watoto, Sh 10,000 kwa wakubwa na Sh 50,000 kwa viti maalumu.

Naye Mwenyekiti wa bongo movie, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ alisema wasanii wavunje tofauti walizonazo na kuungana siku hiyo katika kumuenzi Kanumba.

Kwa upande wake, Mama Kanumba, Mary Mtegoa aliwakaribisha watanzania na wapenzi wa filamu wa Kanumba kujitokeza kushiriki kwa pamoja siku hiyo ili kuenzi kazi zake.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi