loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washambuliwa Nigeria wakitazama Kombe la Dunia

Wakazi wa eneo hilo wanasema walisikia sauti ya mlipuko mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini Damaturu ambapo mashabiki wa soka walikuwa wamejumuika kutazama mechi za Kombe la Dunia.

Walioshuhudia wanasema mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na mgahawa katika Jimbo la Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea.

Yobe imekumbwa na mashambulizi ya Boko Haram katika miaka iliyopita. Habari kutoka hospitalini zinasema malori kadhaa yalitumika kusafirisha majeruhi kwa ajili ya matibabu na polisi wanasema maofisa wamepelekwa katika eneo hilo.

Mfanyakazi mmoja wa hospitali alilieleza Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na mikono.

Wiki iliyopita maofisa wa utawala katika Jimbo la Adamawa ambalo liko katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria walipiga marufuku watu kujumuika katika maeneo ya umma kutazama mechi za Kombe la Dunia kutokana na hofu ya usalama.

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya shambulio kutokea katika eneo la burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.

Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika hali ya tahadhari tangu mwaka 2013 kufuatia mashambulizi yanayofanywa kila mara na wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Boko Haram.

Takribani watu 2,000 wamepoteza maisha kutokana na matukio ya kushambuliwa tangu mwaka 2009.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Nigeria, Junior Lokosa ametua ...

foto
Mwandishi: LAGOS, Nigeria

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi