loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washauriwa kunadi utalii wa utamaduni

Ushauri huo ulitolewa kutokana na mapango ya utalii ya Amboni mkoani hapa, kutopata watalii wengi. Aidha, imeelezwa taarifa zilizohusisha mapango hayo ya utalii na tukio la uhalifu la hivi karibuni, ziliathiri ujio wa watalii katika mapango hayo licha ya kwamba matukio husika, yalijitokeza eneo tofauti na eneo hilo.

Akitoa maelezo juzi kwa watalii waliotaka kufahamu hali ya ujio wa wataalii kutembelea eneo hilo, Mhifadhi wa Mambo ya Kale wa Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora, alisema watalii 65 wa ndani na mmoja wa nje mmoja hutembelea mapango hayo kwa mwaka.

Miongoni mwa watalii waliofika eneo hilo juzi, ni timu ya wadau na wataalamu wa Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) ambao walitembelea vituo vyote 13 vilivyo ndani ya pango kuu kushuhudia vivutio vilivyomo.

Mhifadhi huyo alisema eneo hilo la kitaifa la utalii, halitangazwi na kunadiwa kama ilivyo maeneo mengine ya utamaduni yaliyo chini ya dunia kama vile Mji Mkongwe wa Zanzibar, Bagamoyo na Olduvai Gorge pamoja na mbuga za wanyama.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi