loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasingizia ujauzito, waazima ‘vichanga’ kukwepa foleni BVR

Wanaosingizia ujauzito huvaa nguo nyingi mwilini, kutengeneza ujauzito feki kwa lengo pia la kupata kipaumbele katika uandikishaji huo, kwani wajawazito na wazee hawapangi foleni na badala yake wakifika vituoni huruhusiwa kujiandikisha na kupiga picha kisha kuandoka.

Hali hiyo ilishuhudiwa katika vituo venye watu wengi katika eneo la Mbagala, hasa katika mitaa ya Mgeninani, Mwanatiti, Misheni, Mtoni Kijichi na Butiama.

Akizungumzia hali ilivyo katika eneo lake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Butiama, Magafu Michael alisema eneo lake kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, lina wakazi zaidi ya 16,000. Alisema hadi hivi sasa hata robo ya walioandikishwa haijatimia.

Alisema walitarajia kuandikisha watu zaidi ya 6,000. “Hapa kwetu tuna changamoto kubwa ya idadi ya watu, hasa wanaotoka katika maeneo ya majirani zetu, kiasi kwamba hata wanachi wa eneo hili wameshindwa kuandikishwa kwa wingi hadi hivi sasa. Vilevile wengine wanatumia mbinu za kutengeneza ujauzito usio halali ili waandikishwe mapema, kitu ambacho kimekuwa kikizua ugomvi,” alisema Michael.

Gazeti hili lilishuhudia wananchi wengi wakiendelea kupiga kambi huku wengine wakidai wanakesha katika vituo vya kujiandikisha ili kunapopambazuka waweze kuandikishwa mapema.

Katika kituo cha Kongowe, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, majira ya saa 12.30 asubuhi jana, mamia ya wananchi walikuwepo kituoni hapo wakiwa wamepanga foleni kusubiri maofisa waandikishaji kufika na kufungua kituo.

Wakizungumza na gazeti hili, walisema wamewahi ili kuhakikisha wanapata namba za mwanzo ili kuandikishwa na kuendelea na shughuli zingine za uzalishaji mali.

“Nimefika mapema sana kwani juzi nilifika nikakuta kuna watu wengi nikaondoka.Leo nimeamka tangu saa tisa na nimekuta hapa kuna watu kama kumi hivi, hali si shwari, tunaomba serikali iongeze mashine ili kuongeza kasi ya uandikishaji,” alisema Elisante Jonas, aliyefika kujiandikisha katika kituo cha Mzinga.

Katika kituo cha Kongowe Mwisho, kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliofika kituoni hapo huku waliokuwa wakihudumiwa ni wale waliojiandikisha siku mbili zilizopita kutokana na kushindwa kuandikisha kwa siku moja na kupata kitambulisho kwa siku hiyo hiyo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imempandisha kizimbani ...

foto
Mwandishi: Emmanuel Ghula

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi