loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasira amtaka Lisu aombe radhi maaskofu, mashehe

Aidha, Wasira pia amemtaka msemaji wa Ukawa, Tundu Lisu kuwaomba radhi mashehe na maaskofu ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kwa kudai ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wamekuwa wakihongwa chakula, chai na fedha katika nyumba za viongozi.

Alitoa maoni hayo jana kwenye mdahalo wa Tanzania Tuitakayo uliolenga kuangalia ‘Nani anataka kuwazuia Watanzania kupata Katiba Mpya,” akiwa sambamba na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Profesa Ibrahim Lipumba na Lissu.

Alisema kama Ukawa wanaungwa mkono na wananchi, ni vyema watumie nafasi hiyo kurejea bungeni na kujadili rasimu ndani ya Bunge na baadaye wasubiri wananchi waamue.

“Kama wanachokiamini Ukawa kuwa wako pamoja na wananchi, kwanini wanakwenda kwa wananchi kabla hawajamaliza kazi. Warejee bungeni tujadiliane na kumaliza kazi halafu wakatushitaki kwa wananchi, tuone Ukawa watapata ngapi… kwanini tuandikie mate na wino upo?”

Aliongeza: “Kama ni muundo wa serikali mbili au tatu utajulikana bungeni.” Wasira alisema Ukawa wanatakiwa kujua kuwa sheria inataka Katiba kuandikwa ndani ya Bunge na si sehemu nyingine na kushindwa kufanya hivyo ni kukwamisha mchakato huo ambao umefikia hatua ya tatu.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi