loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watafiti, wataalamu kukutana kujadili utumiaji wa rasilimali

Mkutano huu wa wataalamu utakaowajumuisha washiriki kutoka Afrika na sehemu nyingine za ulimwengu, ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 na Kongamano la Mwaka la Utafiti la Taasisi Inayoshughulika na Utafiti wa Kupunguza Umaskini (Repoa).

Kaimu Mkurugenzi wa Repoa, Dk Donald Mmari alisema majadiliano yatahusu mifano na mikakati mbalimbali itakayowezesha utumiaji mzuri wa rasilimali za nchi kama vile gesi asilia, mafuta na madini zinanufaisha mamilioni ya Watanzania, Lengo kuu la warsha alisema, “ni kukuza majadiliano ya kisera yanayojikita kwenye ushahidi utokanao na utafiti kuhusu usimamizi mzuri wa rasilimali unaochochea mabadiliko ya kiuchumi ili kupata maendeleo yanayoinufaisha jamii pana zaidi.”

Dk Mmari alisema washiriki wa warsha watafahamishwa aina ya rasilimali ilizo nazo Tanzania na serikali inachagua aina ya uwekezaji na kiwango chake, aina ya tozo na njia za kupunguza athari kwa wadau.

Masuala mengine yatakayojadiliwa na kufanyiwa uamuzi yanahusu matokeo ya utafutaji au utumiaji wa rasilimali na njia mbadala za kuongeza mapato na usimamizi mzuri wa kodi, uhusiano kati ya utumiaji wa rasilimali na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Pia washiriki watajadili upatikanaji wa ajira, mitandao ya usambazaji, upatikanaji wa teknolojia, usimamizi wa mazingira, matarajio, vikwazo na fursa zilizopo kwa mtu mmoja mmoja na kwa makampuni yaliyopo nchini.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi