loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watafuta kazi wafundishwa kupata ajira

Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa Wakala huo, Jamillah Mbarouk wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Akifafanua Jamillah alisema kati ya watafuta kazi waliopatiwa mafunzo hayo wanaume ni 1,254 na wanawake ni 879.

“Vile vile wakala umeweza kutoa mafunzo haya kwa vyuo vitano (5) ambavyo ni Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Taasisi ya Uhasibu (TIA), Chuo cha Ardhi na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ambapo vyuo vyote viko Dar es Salaam na kushirikisha wanavyuo 860,” alisema Jamillah.

Kwa sasa mafunzo haya hutolewa kila Ijumaa kwa watafuta kazi waliosajiliwa TaESA. Katika kutoa mafunzo hayo TaESA imelenga kuwajengea uwezo watafuta kazi, kuwajengea uwezo na ujuzi wa kuandika barua za maombi ya kazi, jinsi ya kufanya usaili kwa kujiamini na kuelewa kuhusu matarajio ya waajiri kwa wafanyakazi.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Frank Mvungi – MAELEZO

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi