loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wataka mapori ya akiba yatumike kufugia nyuki

Hayo yalisemwa leo na watafiti wa masuala ya ufugaji nyuki nchini wakati wakiwasilisha utafiti wao uliofanyika Julai na Agosti mwaka huu nchini, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa wadau wa asali na nyuki Afrika utakaofanyika Novemba mwaka huu jijini Arusha.

Mtafiti Dk Angela Mwakatobi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori nchini (TAWIRI), alisema katika utafiti wake aliyoufanya mkoani Kigoma, umebaini wanawake wanaojihusisha na ufugaji nyuki ni asilimia 30 huku vijana wakiwa asilimia nane pekee katika kundi la wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35.

Alishauri vijana wawezeshwe mtaji kupitia vikundi kwenye benki za vijijini (Vicoba) na vyama vya akiba na mikopo (Saccos) huku wadau kwa kushirikiana na serikali wakitakiwa kuendelea kutoa elimu kuhusu ufugaji wa kisasa wa nyuki na faida za mazao yake.

Naye Mtafiti na Msimamizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki Wilaya ya Kibondo, Kigoma, Seif Salum, alisema mabadiliko ya tabia nchi yamechangia kuwakimbiza nyuki katika mapori na katika wilaya hiyo uzalishaji wa asali umepungua.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Selestine Gesimba akifungua mkutano wa watafiti hao jana, alisema matokeo ya utafiti saba uliofanyika yatawasilishwa Arusha kupitia mada 25 na kuhusu matumizi ya mapori alieleza kuwa ni suala linalohitaji utafiti zaidi kwa kuwa si kila pori nyuki hukaa.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi