loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wataka marekebisho ya sheria kuwapa haki abiria wa mabasi kudai fidia

Ushauri huo ulitolewa jana na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra CCC) ambalo pia limetaka kampuni za bima kutokumbatia wenye magari yenye bima kubwa inapotokea ajali na kuacha abiria walioathirika.

Katibu Mtendaji wa Sumatra CCC, Oscar Kikoyo alisema hayo akizungumza na mwandishi wa habari juu ya haki na wajibu wa kampuni za bima kulipa fidia kwa waathirika wa ajali hususani wanaopata ulemavu pamoja na wanaopoteza maisha.

Alisema si vyema kampuni za bima kutoa mbinu zitakazowezesha wamiliki wa mabasi kushinda kesi, jambo linalosababisha walioathirika kushindwa kupata haki.

“Kama ndege zinalipa fidia watu waliokufa na meli pia iweje mabasi yakwepe kulipa fidia pale yanapotokea majanga? Na pia hivi sasa tunataka kuomba serikali watupe meno yatakayotusaidia kuwaonesha njia abiria kwa ajili ya kupata fidia,” alisema Kikoyo.

Katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayoadhimishwa kitaifa mkoani hapa, baadhi ya watu walishutumu baadhi ya madereva wa daladala kutozingatia kanuni za usalama barabarani na pia utoaji lugha chafu.

Na Grace Chilongola kutoka Mwanza anaripoti kwamba imeshauriwa serikali ielimishe matumizi salama ya barabara kwa watu wote kuepusha ajali.

Mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki, mkoani Mwanza, Makoye Kayanda pamoja na madereva wengine, walisema ajali nyingine zimekuwa zikisababishwa na watu wasio na uelewa na hivyo kuwachanganya madereva na hatimaye kutokea ajali.

“Sheria za barabarani hazibagui na zinahitajika kutolewa kwa watu wote wanao tumia barabara,” alisema Salum Miraji ambaye ni dereva wa Hiace.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi