loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wataka sheria ziwabane waharibifu wa mazingira

Hayo yalisemwa jana baada ya maandamano ya wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Dar es Salaam kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.

Jana duniani kote kulikuwa na maandamano ya aina hiyo ili kuwasilisha ujumbe kwa viongozi wa nchi ambao kesho watahutubia katika Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu mabadiliko hayo na kila nchi inavyolishughulikia suala hilo.

Maandamano hayo ya amani yaliandaliwa na taasisi zisizo za kiserikali za Oxfam, Forum CC na Youth Can kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe kwa Serikali ili kupiga vita vyanzo vya mabadiliko ya tabia nchi.

Wanafunzi hao walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali unaopiga vita uharibifu wa mazingira na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi katika upatikanaji wa chakula.

Wanafunzi hao waliitaka Serikali kuweka sheria zinazozuia uharibifu wa mazingira na kusimamia utekelezaji wa sheria hizo, ili kuwa fundisho kwa watu kama hao.

Mmoja wa wanafunzi hao, Hamis Said anayesoma Shule ya Sekondari Jitegemee alisema Serikali itoe elimu kwa raia wake juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Naye Mwakilishi wa Oxfam Eliuka Kibona alisema kuwa lengo la mkusanyiko huo ni kutoa mwito kwa viongozi wa nchi zinazoendelea kufanya kiujasiri mipango ya utekelezaji kwa ajili ya kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Pia alisema nchi zinazoendelea lazima zikubali kubuni njia za kupunguza hewa ukaa ambayo itasaidia kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa hivyo kuboresha mazingira.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi