loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watakiwa kuchangamkia fursa za biashara

Akizungumza jana wakati wa mkutano wa Wizara ya Viwanda na Biashara juu ya kazi zilizopewa kipaumbele katika mpango wa utekelezwaji kwa mwaka 2014/15, Ofisa Biashara Mwandamizi, Prisca Mbaga alisema fursa za biashara zipo nyingi kikubwa ni wafanyabiashara kuzichangamkia.

Alisema kwa sasa nchi zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa wafanyabiashara kupeleka biashara zao hakuna ushuru wowote watakaodaiwa hivyo ni vyema wafanyabiashara hapa nchini kutumia nafasi hii kujitangaza na kutangaza biashara zao Kimataifa.

Alisema wafanyabiashara ili waweze kujitangaza vizuri ni vyema wakapeleka bidhaa zenye ubora uliodhibitishwa na sio bidhaa zilizopo chini ya viwango.

Aliongeza kuwa kwa mfano China imesaini mkataba wa biashara na Tanzania na wamekubaliana kutoa punguzo la hadi asilimia 97 kwa biashara kutoka Tanzania kuingia nchini humo bila kutozwa ushuru wala kuwekewa ukomo jambo ambalo ni gumu kutokea kwa nchi nyingine.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Athuman Nkungu alisema kazi ambazo wamezipa kipaumbele kwa mwaka 2014/15 ni pamoja na kuongezeka kwa uwekezaji ambapo serikali inaendelea kufufua na kuendeleza viwanda vya ngozi kwa lengo la kuongeza thamani ya ngozi kuliko kuuza ngozi ghafi.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi