loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Watanzania wahimizwa kufanya mazoezi

Amesema kwa mujibu wa utafiti, zaidi ya asilimia 9.1 ya Watanzania wanaugua ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk Stephen alisema leo Tanzania inaungana na dunia nzima kuadhimisha Siku ya Kisukari. Hata hivyo alisema watu wengi hawajitambui kwamba wanaugua ugonjwa huo.

“Kama nilivyosema watu wengi hawajitambui kuwa wana ugonjwa huu, wengine wanakuwa na dalili lakini hawachukui hatua mapema, ni vizuri ukiwa na dalili kwenda hospitali mapema ukapime kisukari,” alisema Dk Stephen.

Alisema asilimia 80 ya wagonjwa wa kisukari duniani, wanaishi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana kulikuwa na wagonjwa milioni 382 duniani kote na ifikapo mwaka 2035 inatarajiwa kuwa na wagonjwa milioni 592.

Aidha, alisema kwa Tanzania utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 nchini ulionesha asilimia 9.1 ya watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari.

Alisema takwimu za watoto wenye kisukari mwaka huu ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wote wanaotibiwa nchini, ambapo kwa mwaka gharama ya kutibu mgonjwa mmoja ni Sh 408,000.

foto
Mwandishi: Regina Kumba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi