loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watendaji tisa wawekwa rumande

Kukamatwa kwa watendaji hao, kunafuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara, Christina Mndeme alilolitoa kwa polisi baada ya watendaji hao kushindwa kutimiza wajibu wao.

Taarifa kutoka wilayani hapo zinasema watendaji hao, walilala kwenye kituo cha Polisi cha Katesh.

Watendaji waliokamatwa na kata zao kwenye mabano ni, Clement William (Nangwa), Jonas Samo (Basodesh), Valentine Manya (Gendabi), Peter Umbe (Hirbadaw), Lala Baraza (Endashul), Ibrahim Jambau (Gisambalang’) Paskalina Gishul (Masqaroda), Akwelin Umbu (Hidet) na Grace Dofa (Ganana).

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya, aliagiza watendaji hao kwamba ifikapo Septemba 15 mwaka huu, wawe wamemaliza kusimamia wananchi wa sehemu husika kukamilisha ujenzi wa maabara lakini wakazembea.

“Watendaji hao walishindwa kusimamia ujenzi huo kwenye kata zao, hivyo nimechukua hatua hiyo kwa lengo la kuwapa changamoto ili wakitoka wahakikishe wanasimamia ipasavyo umaliziaji wa maabara,” alisema Mndeme.

Alisema lengo la wilaya hiyo ni kumalizia vyumba vya maabara zaidi ya 100 lakini hadi sasa ni vyumba 22 pekee vilivyomalizika; jambo linalohitaji jitihada za ziada.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Hanang'

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi