loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

'Watoto 130 hufa kila siku kwa lishe duni'

Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk Rajab Rutengwe.

Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yalifanyika jana kitaifa katika Viwanja vya Kashaulili katika Mji wa Mpanda mkoani Katavi na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wananchi.

“Ni fedheha kubwa kwa nchi yetu kuendelea kukabiliwa na janga la udumavu linalotokana na kukosa lishe bora na matunzo sahihi …ni jambo lisilokubalika wala kuvumilika hata kidogo kuendelea kupoteza maisha ya zaidi ya watoto 130 kila siku kutokana na kukosa lishe bora na matunzo sahihi,“ alibainisha.

Alikumbusha kuwa madhara makubwa yanaweza kutokea katika ukuaji wa kimwili na kiakili kwa mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili jambo la msingi likiwa kuelewa kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara unapoongezeka lazima mkazo uwekwe katika kuboresha lishe katika familia.

Aliongeza kuwa ni jambo lisiloweza kuingia akilini iwapo ongezeko la uzalishaji wa chakula haliwezi kuendana na upunguzaji wa tatizo la utapia mlo na kudumaa kwa watoto ambalo linaendelea kutishia maisha hapa nchini.

Takwimu za 2010 zinaonesha kuwa asilimia 42 ya watoto chini ya miaka mitano wamedumaa huku asilimia 16 wana uzito pungufu na asilimia tano wamekonda asilimia 59 ya watoto kati ya miezi sita na 59 wana upungufu wa damu na asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu mkubwa wa vitamini A.

Kwa mujibu wa takwimu hizo asilimia 11 ya wanawake walio na umri wa kuzaa kati ya miaka 15 na 49 wamekonda, asilimia 41 wana upungufu wa damu na asilimia 58 ya wajawazito wana upungufu wa damu.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Mpanda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi