loader
Watoto wapelekwe kwenye michezo kipindi hiki cha sikukuu

Watoto wapelekwe kwenye michezo kipindi hiki cha sikukuu

LEO ni siku muhimu kwa Wakristo duniani kote, ni sikukuu ya Krismasi (Noeli), ni siku ambayo wengi husheherekea kuzaliwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

Kwa kawaida siku hii husherehekewa Desemba 25, katika Ukristo wa Magharibi na Januari 6 katika ule wa Mashariki.

Sherehe hii duniani kote husherehekewa kwa namna mbalimbali kulingana na mahali walipo, wengine huenda kuwatembelea watu wenye mahitaji maalumu kama wafungwa, wagonjwa na watoto yatima.

Lakini wengine huenda katika majumba ya starehe kunywa na kuangalia filamu. Watoto ni kundi jingine ambalo pia wanatembea 

huku na kule kufurahisha nyoyo zao.

Miaka iliyopita kwa nyakati tofauti katika sikukuu kama hizi kulikuwa kukiripotiwa matukio mbalimbali ya uhalifu hasa upotevu wa watoto kutokana na uzembe wa wazazi au kuwaacha wakatembea wenyewe mitaani, bila ya uangalizi maalumu.

Napenda kutoa rai kwa wazazi, wanapaswa kujifunza kutokana na matukio yaliyopita kwa kuwa makini na watoto hususani pale wanapoamua kuwaruhusu watembee wenyewe.

Lakini pia wanapaswa kuitumia siku hii kusherehekea kwa kufanya mambo yanayowaletea faida na kujiepusha na mambo ya uvunjifu wa amani.

Hasa kwa wakazi waishio mijini, ndio wapo katika maeneo yanayohitaji uangalizi mkubwa kwa watoto kwani wanakuwa na utaratibu wa kwenda sehemu ambazo zina mikusanyiko ya watu wengi, kama hakuna mtu wa kuwasimamia ni

rahisi kwa wao kupotea na kusababisha usumbufu kwa vyombo vya usalama.

Hivyo, wazazi wote wanapaswa kuelewa umuhimu wa huzingatia usalama wa watoto wao hususani siku kama ya leo pindi wanapowaruhusu vijana wao kutoka nje ya mazingira ya nyumbani.

Aidha, kwa upande wa wanaoandaa sehemu za michezo ya watoto ambayo ni moja ya kukamilisha furaha ya watoto kwa kusherehekea sikukuu, wanapaswa kuweka utaratibu maalumu wa kuwazuia watoto wasizurule, pasi na muongozo.

Rai yangu kwa Jeshi la Polisi, kuwausia wazazi kuwa makini na watoto wao hasa siku kama ya leo pindi wanapotoka majumbani kwenda kusherehekea hasa kwenye ufukwe wa bahari.

Litakuwa jambo zuri endapo Jeshi la Polisi litaelekeza nguvu zaidi katika maeneo yanayotazamiwa kuwa na msongamano mkubwa wa watu katika kipindi hiki cha sikukuu ili kuwahakikishia usalama wao.

Pia Watanzania wanapaswa kuwa makini na mali zao hasa leo kwani nyakati kama hizi ndipo vitendo vya wizi hushamiri.

Lakini pia katika kipindi hiki cha sikukuu kumekuwa na matukio mengi ya uporaji, katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi hivyo Watanzania mnapaswa kuwa makini hasa nyakati hizi za mwisho wa mwaka.

Hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anakuwa makini na kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa amani kwa wengine vinavyoweza kumsababishia matatizo yasiyokuwa na ulazima.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c631ec95512b59b8a630fcab0cf13ec8.png

SERIKALI kupitia Shirika ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi