Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika Mjini Kahama yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao wa kufanya kazi kutoka katika mfumo huo wa zamani wa karatasi kwenda katika mfumo wa Kompyuta unaotumiwa na taasisi nyingi kwa sasa hapa duniani.
Mwezeshaji wa Semina hiyo kutoka idara ya Mahakama makao Makuu, Samweli Fredrick alisema mafunzo hayo yatasaidia kupata ripoti kwa urahisi.
Alisema kuwa mfumo wa karatasi uliokuwepo awali ulikuwa ukiwawia vigumu kupata taarifa kwa haraka pindi zinapotakiwa.
Kwa upande wake Mratibu wa Semina hiyo, Gadiel Marick alisema kuwa semina hiyo imewashirikisha washiriki 32 kutoka katika Wilaya za Bukombe na Kahama na kuongeza kuwa mafunzo hayo yanatarajia kuleta mabadiliko makubwa ya utendaji wa kazi katika idara ya mahakama.