loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watumishi washauriwa kusoma sheria za kazi

Mwito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Katibu wa Chama cha Umoja wa Wafanyakazi wa Viwandani na Biashara (TUICO) mkoani Tanga, Martin Wawa wakati wa hafla ya kusaini toleo la pili la mkataba wa hali bora ya kazi mahali pa kazi.

Mkataba huo ulisainiwa baina ya Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi, Majitaka na Usafi wa MazingiraTanga (UWASA) na wafanyakazi wanaounda tawi la Tuico kwenye mamlaka hiyo.

Alisema uzoefu unaonesha kwamba idadi kubwa ya watumishi hawana mazoea ya kupitia sheria mbalimbali za kazi pamoja na kanuni zake hatua inayosababisha washindwe kutofautisha haki na stahili zao kabla ya kuzidai kutoka kwa mwajiri.

“Sina hakika kama baadhi ya watumishi hapa wanafahamu kwamba asilimia 90 ya sheria zote za kazi zinazotumika hapa nchini zimeondoa kipengele cha maslahi hasa baada ya sheria ya mwaka 2004 kufuta maslahi mbalimbali kwa kuacha mwanya wa majadiliano ya kupata mkataba wa halibora kazini”, alisema Wawa.

Aidha aliongeza,“Unapofungwa mkataba wa hali bora mahali pa kazi hiyo ndiyo inageuka sheria ya kumpa mtumishi haki ya kudai maslahi mbalimbali waliyopatana … kama mfanyakazi hatakuwa na uelewa kama huo itakuwa vigumu sana kwake kwenda kumdai mwajiri mafao ya matibabu, maziko na mengineyo kwa sababu hayamo kwenye sheria ya kazi”, alisema.

Akizungumzia mkataba huo uliofungwa baina ya chama hicho na menejimenti ya Uwasa aliwapongeza na kusema ni hatua nzuri ya mafanikio iliyofikiwa.

Awali akizungumzia kwa niaba ya menejimenti ya Uwasa, Meneja Rasilimaliwatu, Haika Ndalama alisema kusainiwa kwa mkataba huo kumeiingiza mamlaka katika ramani ya taasisi ambayo ni ‘mwajiribora’ Tanzania.

Naye Mwenyekiti wa tawi la Tuico la Uwasa, Shabani Shekue alisema mkataba huo umeanza kutekelezwa Novemba mwaka jana baada ya kuboreshwa kwa mambo makuu mawili yakiwemo mafao ya wastaafu na msiba na kwamba kuhusu malipo ya posho na motisha vitatekelezwa kuanzia Julai mosi mwaka huu.

MWENYEKITI wa Taasisi za Sekta Binafsi ...

foto
Mwandishi: Anna Makange, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi