loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watupwa jela kwa kuishi karibu na chanzo cha mto

Hakimu wa mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalira amewahukumu watu saba kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja, wanne wamehukumiwa kutumikia kifungo cha nje mwaka mmoja kila mmoja wao na wengine kumi wameachiwa huru .

Akisoma hukumu hiyo Rugemalira alisema washtakiwa hao 11 wamevunja sheria ya hifadhi ya mazingira ya halmashauri ya wilaya Nkasi ya mwaka 1997 kifungu cha 3 namba 4 kifungu kidogo cha 3 kinachokataza watu kuishi na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ndani ya chanzo cha maji.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali za Mitaa mkoani Rukwa, Tulalemwa Mwenda ni alidai mahakamani hapo washitakiwa hao walivamia chanzo hicho cha maji kwa kujenga makazi yao na kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kwa kufuga mifugo na kuhatarisha chanzo hicho cha maji.

Waliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela ni pamoja na Japhet Jilala, Alexander Swahila, Agape Matemba, Dotto Charles, Egydi Mizimu Galisto Mafuso na Julius Mpepo ambao walitiwa hatiani kwa kosa la kwanza kati ya mawili waliyokuwa wakikabiliwa nayo ya kuishi na kufuga ndani ya chanzo cha maji kinyume cha sheria.

Wanne waliofungwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja na wasiweze kufanya kosa lolote ni pamoja na Lalenda Machile, Mashaka Kifundo, Emmanuel Mpepo na Japhet Matemba.

Walioachiwa huru kwa kutopatikana na makosa yoyote ni pamoja na Fredrick Makanta, Vicent Katalila, Kanele Ndungumila, Kulwa Makena, Gingu Chilala na Maduhu Antony, Leonard Mwami, Vitus Tuseko, Michael Zeno na Juma Makoso.

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Namanyere

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi