loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wauawa wakituhumiwa kuvua kwa sumu

Kwa mujibu wa Kamanda Mlowola, mauaji hayo yalifanyika katika Kijiji cha Msozi juzi saa 5 usiku na wengine wawili wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya, mjini Nansio. Waliouawa ni Hassan Rashid (30), mkazi wa Mjini Nansio na Mafele Mbuganalwa (40), mkazi wa Kijiji cha Buramba.

Kwa upande wa waliolazwa hospitalini, ambao wametajwa kuwa hali zao ni mbaya, ni Kulunya Mzegezo (46) na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Seleman.

Kamanda Mlowola alisema wavuvi hao walivamiwa na kushambuliwa na kundi kubwa la wananchi muda mfupi baada ya mtumbwi wao kutia nanga kijijini hapo.

Mashuhuda wa tukio hilo, walidai kwamba wavuvi hao waliwekewa mtego baada ya wananchi kuwatuhumu kwa muda mrefu kwamba wanatumia sumu kuvua samaki.

Hata hivyo taarifa kutoka Polisi zilisema, wavuvi hao walikuwa na shehena kubwa ya samaki.

Pia ndani ya mtumbwi, kulikutwa chupa sita zenye sumu aina ya Thiodan pamoja na nyavu haramu aina ya Timba.

Kamanda Mlowola alisema wakati uchunguzi ukiendelea, msako unaendelea kubaini waliohusika katika mauaji hayo na kujeruhi.

Alisema msaada mkubwa wa kuwapata watuhumiwa, utatokana na maelezo ya waathirika wanaotibiwa hospitalini.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: Jovither Kaijage , Ukerewe

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi