loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wavuvi wadogo kupewa ruzuku

Mbunge huyo alihoji kwa nini Serikali haitoi kipaumbele kwenye sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha wavuvi wadogo kupata zana za kisasa.

Waziri huyo alisema katika Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (Mkukuta), sekta ya uvuvi imeendelea kupewa kipaumbele ambapo Serikali kupitia programu ya kuendeleza sekta ya uvuvi, imeainisha maeneo ya utekelezaji unaolenga kuwa na uvuvi wenye tija.

Alitaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni kuimarisha usimamizi shirikishi wa rasilimali na uvuvi, kuimarisha masoko na usalama wa mazao ya uvuvi na kuboresha elimu ya uvuvi endelevu.

Maeneo mengine ni pamoja na kuendeleza ukuaji wa viumbe kwenye maji, kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi na kuboresha utaalamu wa matumizi ya teknolojia sahihi, ili kufanya uvuvi na ufugaji samaki uwe na wenye tija.

Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, imekuwa ikibuni na kutekeleza miradi mbalimbali, ambayo ni pamoja na Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Bahari ya Ukanda wa Pwani (MACEP), uliotekelezwa kwa mwaka 2005 hadi 2012. Alisema wavuvi wadogo 4,000 waliwezeshwa kutekeleza miradi ya uvuvi 240 yenye thamani ya Sh bilioni 3.8.

Aidha, wavuvi 634 wanaoishi katika hifadhi za bahari za Mafia na Ghuba ya Mnazi na maingilio ya mto Ruvuma, walipewa ruzuku ya kununua injini a boti 22, madema 20, maboya 26,000, boti 28 za uvuvi na nyvu 1,403 zilizogharimu Sh milioni 339.3.

Pia, Waziri huyo alisema, serikali kupitia DADP’s kwenye halmashauri ya Ludewa ilitoa Sh milioni 59.7 kwa vikundi vinane kwa ajili ya kununulia injini, boti na zana za uvuvi na inajenga kiwanda cha kutengeneza boti Mbamba Bay (Mbinga) ili kuwawezesha wavuvi wadogo kupata boti imara na zana bora za uvuvi.

Alisema katika mwaka wa fedha 2013/2014, serikali itaanzisha mfumo wa kutoa ruzuku kwa wavuvi wadogo, itakayotolewa kwa utaratibu wa Mfuko wa Mzunguko.

Alisema ruzuku hiyo itatumika kununua boti za uvuvi na viambata vyake na zana bora za uvuvi. Pia, ruzuku itatolewa kwa vikundi vya wavuvi vilivyosajiliwa na vinavyofanya shughuli za uvuvi, ambapo chini ya utaratibu huo boti 50 na viambata vyake pamoja na vyavu za uvuvi 15,562 vitatolewa kwa wavuvi.

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi