loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wawekezaji Mkinga wahimizwa kujikita kwenye majengo

Utekelezaji wa uwekezaji huo utawezesha wageni wanaohamia wakiwemo watumishi zaidi ya 100 walioajiriwa kwenye halmashauri ya Mkinga iliyoanzishwa miaka saba iliyopita kupata maeneo mazuri ya kupangisha tofauti na hali ilivyo sasa.

Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa halmashauri ya wilaya ya Mkinga, Amina Kiwanuka ametoa mwito huo alipozungumza jana katika mahojiano na gazeti hili kuhusu utekelezaji wa maagizo mbalimbali yaliyotolewa na viongozi kadhaa wa serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Katikati ya mwaka jana wakati wa ziara yake wilayani Mkinga, Rais Kikwete aliuagiza uongozi wa wilaya hiyo kununua nyumba 40 zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo la Kasera ili kuwapatia makazi watumishi ambao kwa muda mrefu wamelazimika kuendelea kuishi jijini Tanga umbali wa kilomita 60 kutoka kwenye kituo chao cha kazi jambo ambalo linakwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: Anna Makange, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi