loader
Picha

'Wawekezaji wazawa wapewe kipaumbele'

Mtewele alisema hayo leo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopo Sinza.

Alisema ni vyema Serikali ikawaunga mkono wawekezaji wazawa kuliko wa nje ili vijana wengi wenye malengo watumie fursa hiyo kujiajiri wenyewe na kuleta maendeleo ya nchi.

“Unapomuwezesha mzawa nchi inakuwa na wawekezaji wengi kutoka ndani, pia tunaleta maendeleo ya nchi kwa kuwa tunatoa ajira kwa vijana na kulipa kodi, ” alisema Mtewele.

Aliongeza kuwa, katika uwekezaji kuna changamoto mbalimbali hasa sekta zinazohusika kutowasaidia wawekezaji wazawa na kutoa kipaumbele kwa wageni, jambo ambalo linakatisha tamaa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, Ofisa Utumishi Mkuu wa Wilaya hiyo, Godfrey Mgomi alisema sera na sheria hazimzuii mtu kuwekeza bali kuna utaratibu anatakiwa aufute.

Aliwataka vijana kutumia fursa zilizopo kufanya uwekezaji, kama alivyofanya Mtewele ambaye amejenga hoteli na kutoa ajira kwa watu 21 pamoja na kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi