loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wawili hawajaripoti Twiga Stars

Akizungumza baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jana Kocha Mkuu wa timu hiyo Rogasian Kaijage alisema kuwa Evelyn Sekikubo anakabiliwa na mitihani lakini Aziza hana taarifa zake.

“Tumeingia kambini tangu juzi na kuanza mazoezi wachezaji wawili ndio pekee hawajajiunga na kambi kwani niliita wachezaji 30,” alisema Kaijage.

Twiga Stars itaivaa Zambia katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano ya mchujo ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayofanyika Februari 15 mwaka huu jijini Lusaka.

Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Nkoloma na itachezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga kutoka Rwanda akisaidiwa na Wanyarwanda wenzake, Francine Ingabire, Sandrine Murangwa na Angelique Tuyishime. Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Jackey Gertse kutoka Namibia.

KLABU ya Chelsea imemtangaza ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi